Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4673

BUNGE LA TANZANIA KUTOA AZIMIO LA NELSON MANDELA LEO...

$
0
0

Nelson Mandela akiapishwa kuwa Rais wa kwanza mweusi aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini.
Kutokana na kifo cha Rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela,  Bunge la Tanzania leo litatoa maazimio ya kumsifu na kumpongeza, kutokana na ukombozi wa bara la Afrika. 

Hayo yalisemwa jana na Spika, Anne Makinda baada ya Mnadhimu wa Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kutaka Bunge liahirishwe kutokana na kifo cha kiongozi huyo. 
Lissu alisema msiba wa Mandela ni wa bara zima hivyo ni vema Bunge lingeahirishwa hata kwa siku moja ili kumuenzi kiongozi huyo.  
Makinda alisema Bunge linafanya kazi kwa misingi ya sheria na taratibu za nchi, hivyo kwa kuthamini mchango wa kiongozi huyo leo litatoa azimio. Awali wakati wa kuanza kwa kikao cha Bunge, wabunge walisimama kwa muda ili kumwombea kiongozi huyo. Wakati huo huo, Spika Makinda jana alitetea mawaziri na naibu mawaziri wa wizara  ambao hawakuhudhuria kikao cha Bunge wakati wizara zao zikitakiwa kujibu maswali. Alisema ana taarifa za mawaziri na manaibu wao baada ya kuomba udhuru kwa Waziri Mkuu na kila aliyejibu alifanya hivyo kwa niaba ya Serikali. 
 Hatua hiyo ilitokana na Mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) kwa kanuni ya 68 (7) kuhusu mawaziri kutokuwapo na maswali kujibiwa na wizara zingine tena chini ya kiwango. 
Makinda alisema suala la msingi ni kutolewa majibu sahihi kutokana na kuwa yanatolewa na Serikali na kujibiwa na waziri asiye wa wizara husika si sababu ya kutolewa majibu yasiyoridhisha. 
Hayo yalitokea baada ya kuulizwa swali la Wizara ya Nishati na Madini, lakini likajibiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Charles Kitwanga. 
Hatua hiyo ililalamikiwa kutokana na wizara hiyo kuwa na mawaziri watatu na wote kutohudhuria licha ya kufahamu kuwa swali lao linatakiwa kujibiwa siku hiyo. 
Katika swali hilo, Mbunge wa Kibiti, Abdul Marombwa (CCM) alitaka Wizara hiyo kueleza ni lini umeme unaotoka Somanga Fungu utatolewa Bungu, Kwawa, Uponda, Njawa, Jaribu Mpakani hadi Kilimahewa ili kuunganishwa na Gridi ya Taifa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4673

Latest Images

Trending Articles