![]() |
Mzee Nelson Mandela. |
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma alisema usiku huu "Baba huyo wa Taifa" wa Afrika Kusini amefariki akiwa na umri wa miaka 95.
Akihutubia taifa kwa njia ya televisheni, Zuma alisema: "Taifa letu limepoteza mtu muhimu mno. Watu wetu wamempoteza baba.
"Kilichomfanya Mandela kuwa mashuhuri kilikuwa kile kilichomfanya hasa yeye kuwa mwanadamu. Tunaona kwake kile tunachohitaji mioyoni mwetu."
Rais Zuma alisema "taifa limempoteza mtu wake muhimu mno", na kuongeza "sasa amepumzika. Sasa yuko peponi."
Mzee Mandela atafanyiwa mazishi ya kitaifa na bendera za taifa zitapepea nusu mlingoti.
Waziri Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa Mzee Mandela, akisema: "Taa imezima katika dunia. Nelson Mandela alikuwa shujaa wa wakati wetu. Nimeagiza bendera kwenye ofisi Namba 10 zipepee nusu mlingoti."
Mnamo Aprili mwaka huu, mtangazaji wa serikali alirusha hewani video fupi ya Baba huyo wa Taifa aliyedhoofika akiwa ametembelewa na Rais Zuma na maofisa wa juu kutoka chama cha African National Congress.
Mzee Mandela anakumbukwa zaidi kama Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, bondia wa zamani, mwanasheria na mfungwa Namba 46664.
Mungu ailaze roho ya Mzee Madiba mahali pema peponi, Amina.
Habari zaidi zitakujia hapa hapa muda mfupi ujao.