Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4621

PINDA AKANA KULIPWA MSHAHARA MILIONI 30, ASEMA ANALIPWA MILIONI 6/-...

$
0
0
Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amevunja ukimya na kuweka hadharani mshahara wake kuwa ni Sh milioni sita na si milioni 30 kwa mwezi kama inavyopotoshwa.
Pia amesifu mfumo unaotumika nchini wa Serikali kuwapa nyumba watumishi wake wakiwamo viongozi wakuu hali inayowapa nafasi ya kutumikia zaidi wananchi badala ya kushughulikia mambo binafsi.
Pinda alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mohammed Mnyaa (CUF) aliyetaka maelezo kuhusu taarifa za kwenye mitandao kuhusu mshahara wa Rais kuwa ni Sh milioni 32 na Waziri Mkuu Sh milioni 30 kwa mwezi.
“Kwa mujibu wa Katiba, Rais atalipwa mshahara, posho na kiinua mgongo yakiwamo malipo ya uzeeni baada ya Bunge kuidhinisha, sijawahi kusikia Bunge hili likizungumzia jambo hili, lakini pia taarifa za suala hili zimezagaa kwenye vyombo vya habari hauoni kama Bunge limepokwa haki yake?” Alihoji.
Akijibu swali hilo, Waziri Pinda, alikiri kusikia taarifa hizo za mshahara wa Rais na wa kwake kupitia Mbunge wa Kigoma Kaskazini,  Kabwe Zitto (Chadema), kuwa analipwa mshahara wa Sh milioni 30, jambo ambalo lilimshangaza.
“Naomba niweke wazi, mimi Waziri Mkuu napata mshahara wa Sh milioni sita tu kwa mwezi, ambazo ni pamoja na posho ya mke wangu, sasa mtu akiibuka na kusema mengine sijui anataka au anamaanisha nini au labda ni njama!” Alihoji Pinda.
Aliongeza: “Huyu baba wa watu aliyesema haya namwombea kwa Mungu amwepushe na balaa kwa kusema uongo.”
Alisema asingependa kuzungumzia mshahara wa Rais au wa Makamu wa Rais ila alibainisha kuwa tofauti ya mshahara wake na wa viongozi hao wawili haizidi Sh milioni moja.
Alisema pamoja na mshahara wake huo, pia amekuwa akilipwa posho ya Sh 500,000 na Bunge kwa nafasi yake ya uwaziri mkuu akiwa bungeni.
“Lakini pia naomba niweke wazi kuwa kama kuna fundi wa kukopa benki basi mimi ni fundi sana. Nimekopa benki za NMB na CRDB na hata hapa bungeni baada ya kutolewa kwa fursa kwa kukopa asilimia 50 ya kiinua mgongo cha mbunge, miye tayari nimeshaikopa hiyo asilimia 50,” alisisitiza.
Alisifu mfumo uliopo wa kuwapa nyumba za kuishi na chakula bure viongozi wa juu jambo ambalo linawafanya wawajibike ipasavyo na kutojiingiza kwenye tamaa zisizo na maana.
Katika swali la msingi la Mnyaa, alisema kwa mujibu wa Katiba ibara ya 43 inayozungumzia masharti ya kazi ya Rais, ukiwamo mshahara wake, fedha za uzeeni na mafao yake ya kustaafu, ambavyo vyote hutolewa na Mfuko wa Hazina ni lazima kuidhinishwa na Bunge, na kuhoji iwapo Bunge hilo limeshawahi kuidhinisha malipo hayo.
Akijibu swali hilo, Pinda  alikiri kuwa hakujiandaa na swali hilo na kwamba alishtukizwa, hivyo hawezi kuthibitisha bungeni hapo iwapo yalijadiliwa na kupitishwa na Bunge au la.
Hata hivyo, alisema anachofahamu ni kwamba kuwepo kwa kifungu hicho katika Katiba ni lazima sheria ya kuweka utaratibu wa utekelezaji wake iwepo.
“Naamini kuwa mahali fulani lazima kutakuwa na utaratibu uliowekwa na kubainisha mishahara ya viongozi,” alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4621

Trending Articles