Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

VIGOGO WATANO WA POLISI WAVISHWA VYEO...

$
0
0
IGP Said Mwema akimvisha cheo Thobias Andengenye.
Maofisa watano wa Jeshi la Polisi nchini wamevishwa vyeo huku wanane wakiapishwa baada ya kupandishwa vyeo na kuteuliwa juzi na Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
Viongozi hao wa Polisi walivishwa vyeo hivyo na kuapishwa jana na Mkuu wa Jeshi hilo nchini, Said Mwema jijini Dar es Salaam
Maofisa waliovishwa vyeo kutoka Naibu Kamishina wa Polisi kuwa Kamishina wa Polisi ni Hamdani Makame, Thobias Andengenye, Abdulrahman Kaniki na Ernest Mangu. Aliyevishwa unaibu Kamishina wa Polisi ni Diwani Athumani kutoka  Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi.
Walioapishwa ni Kamishina wa Polisi (CP) Clodwig Mtweve ameapishwa kuwa Kamishina wa Fedha na Usafirishaji, CP Paulo Chagonja kuwa Kamishina wa Operesheni na Mafunzo, CP Mussa Ally Mussa kuwa Kamishina wa Polisi Jamii na CP Makame kuwa Kamishina wa Polisi Zanzibar.
Wengine ni CP Issaya Mngulu kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), CP Andengenye kuwa Kamishina wa Utawala na Utumishi, CP Kaniki kuwa Kamishina wa Uchunguzi wa Sayansi ya Makosa ya Jinai na CP Mangu kuwa Kamishina wa Intelijensia ya Makosa ya Jinai.
Mwema alimshukuru Rais Kikwete kwa kutambua na kuthamini mchango wa Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Aidha, Mwema alipongeza waliopandishwa vyeo na walioteuliwa na kusema kupitia vyeo na nyadhifa hizo ni lazima Watanzania waendelee kuwa salama, vitendo vya uhalifu visiwe kikwazo cha jamii kujiletea maendeleo na kuhakikisha usalama unashuka hadi ngazi ya familia.
Wakati huo huo, Rais Kikwete jana alimteua Johari Masoud Sururu, kuwa Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huu ambao unaanzia Novemba 24 mwaka huu, Sururu alikuwa Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania jijini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).
Kutokana  na uteuzi huu, aliyekuwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Mwinchumu Hassan Salim sasa atapangiwa kazi nyingine.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

Trending Articles