![]() |
Josephat Gwajima. |
Wakati viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo nchini wakionekana kushindana kwa utajiri, hali inayowafanya waishi `kifalme' na kufungua miradi mbalimbali, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema kamwe hana mpango wa kufungua biashara, zaidi ya kujikita katika kuhubiri injili.
Aidha, amesema Mungu anaendelea kumbariki katika kazi yake, ndiyo maana mambo yake yanamnyookea, akitolea mfano kubwa baada ya kumiliki nyumba, magari na fedha za kutosha, sasa amembariki na kumpatia helikopta atakayoitumia kuwafikia waumini wake wa ndani na nje ya nchi.
Usafiri huo wa angani utaongeza idadi ya vyombo vya usafiri kwa Mchungaji huyo ambaye anatajwa kuongoza kwa utajiri miongoni mwa viongozi wa madhehebu ya Kikristo nchini, kwani anamiliki magari kadhaa likiwamo la kifahari aina ya Hummer lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 200.
Akizungumza na mwandishi juzi kwa simu, Gwajima ambaye hivi sasa anaendesha mikutano ya kueneza neno la Mungu katika mikoa mbalimbali ikiwemo Kilimanjaro na Tanga anakomaliza leo, alisema tayari helikopta imeshanunuliwa na matarajio yake ni kwamba, baada ya kukamilika taratibu zote za kisheria za hapa nchini, itafika.
"Sipendi kusema mambo yangu sana, lakini kwa kuwa umeuliza naweza kugusia kidogo, ni kweli nina mpango wa kuanza kuhubiri injili kwa helikopta, na kama ilivyo kwa gari, nayo hii nimepewa na watu wa Mungu walioguswa na huduma yangu huko Japan.
"Itafika nchini wakati wowote mambo ya kisheria yakikamilika, huu si wakati wa kuizungumzia sana maana bado haijafika hapa," alisema Gwajima ambaye gari lake aina ya Hummer liliwahi kuzua gumzo, wengine wakimhusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, ingawa amepuuzia madai hayo.
Kuhusiana na helikopta yake ambayo amekataa kutaja aina yake wala thamani, alisema hataitumia kwa shughuli binafsi kwani imetolewa kwa ajili ya kazi ya Mungu hivyo, itakapofika nchini, itafanyakazi ya kurahisisha utoaji wa huduma za kiroho maeneo yasiyofikika nchini.
Mchungaji Gwajima ambaye mara kadhaa amekuwa akielezwa kuwa ni Mchungaji anayeongoza kwa utajiri nchini huku akihusishwa na uuzaji wa dawa za kulevya, mwenyewe alieleza wazi kuwa, utajiri wake unatokana na baraka anazopewa na anaowahudumia ndani na nje ya nchi na pia kazi yake ya kufundisha anayoifanya ughaibuni.
"Siwezi kumzuia mtu asiseme chochote anachodhani anaweza kusema, kama Gwajima atauza unga, basi wauza unga hawapo Tanzania wala duniani, sipendi kujielezea sana wazi mambo yangu, lakini mimi nabarikiwa sana na watu ninaowahudumia nje na ndani ya nchi, pia ninafundisha vyuo vikuu katika karibu miji yote nchini Japan," alifafanua Gwajima.
Akielezea zaidi, alisema anasoma lakini pia ni mwalimu wa theolojia za kiroho wa nje katika vyuo mbalimbali kwenye miji zaidi ya 18 nchini Japan na wanamlipa fedha `nzuri' kwa kazi hiyo ya ziada. Miongoni mwa vyuo anavyofundisha ni Taasisi ya Biblia Japan na Kituo cha Kikristo Tagoshima, vya Japan ambako Machi mwaka kesho anatakiwa kwenda kikazi.
Miji mingine ambayo kuna vyuo anavyofundisha nchini Japan alikodai wanatumia zaidi mafundisho yake, ni pamoja na Tokyo, Osaka, Kobe, Yokohama, Shikoku, Yamaguchi na Sapporo Kusini. Alisema pamoja na kwenda Japan kufundisha, pia kila mwaka wanafunzi 40 kutoka nchini humo huja nchini kujifunza.
Aidha, kutokana na utajiri anaosema unatokana na baraka za Mungu, Mchungaji Gwajima anamiliki jumba la ghorofa nne eneo la Mbezi Beach katika Manispaa ya Kinondoni, ingawa haijakamilika yote.
Pia amewanunulia wachungaji wake 40 magari ya kutembelea kwa bei tofauti, yakiwemo ya chini ya Sh milioni 10 na mengine ya zaidi ya Sh milioni 20.
"Ni kweli nimewanunulia magari, unajua moja ya misingi yangu ya maisha ni kwamba, mimi siwezi kuishi maisha mazuri, wakati wachungaji wangu wanadhalilika, nimewanunulia magari karibia 40. Lakini nina wachungaji wa ngazi mbalimbali, hawa ni wale wa juu, wengine wachungaji wadogo wapo zaidi ya 670, hawa ni watenda kazi muhimu na wanatofautiana kwa ngazi zao, ndio maana kazi ya Mungu inasonga mbele hata nisipokuwepo," alisema Gwajima.
Mbali na magari ya wachungaji, pia amenunua mabasi 20 ya kubeba waumini wake kutoka na kwenda kanisani, yakianzia maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Alithibitisha kuwa, kila moja limegharimu kati ya Sh milioni 80 na Sh milioni 100.
Pamoja na uwezo mkubwa wa kifedha alionao, anasema kamwe hatageukia biashara kwa kuwa hatafuti faida, bali kumtumikia Mungu ambaye naye anampa baraka za kipato alichonacho kwa sasa.
"Kasi ya huduma itakuwa zaidi siku hadi siku kutokana na Mungu ninamuamini na watu ninaofanya nao kazi kuwa waaminifu mbele za Mungu sipo tayari kuchanganya biashara na mambo ya kiroho kwani sitafuti faida," anasema na kusisitiza kuwa, vyombo vya usafiri alivyonavyo ni vya kanisa na hakuna mtu aliyelazimishwa kuchangia ununuzi wake.
Anaongeza kuwa, si yeye binafsi wala kanisa lake lenye ufunuo wa kufungua miradi ya shule, hospitali ama benki na kudai kuwa, makanisa mengine yanafanya biashara na si kutoa huduma, akisema ni gharama kubwa kuendesha shule au hospitali, hivyo kusema wanaofanya hivyo hawana tofauti na wafanyabiashara wengine binafsi.
Mbali ya Mchungaji Gwajima, viongozi wengine wa makanisa wanaotajwa kuwa na utajiri mkubwa wa mali na fedha ni Nabii na Mtume Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha anayemiliki benki, mashamba makubwa na mali nyingine, Mchungaji Gertrude Lwakatare wa Mikocheni B Assemblies of God anayemiliki mtandao wa shule za St. Mary's nchini.
Wengine ni Askofu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Anthony Lusekelo `Mzee wa Upako' wa Kanisa la Maombezi `GRC', na Mtume Onesmo Ndegi wa Kanisa la Living Water Center 'Makuti Kawe'.