![]() |
Viongozi wa Chadema wakishiriki katika moja ya kampeni za chama hicho. |
Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chadema (Chaso) Mkoa wa Dar es Salaam, umeunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho wa kuwavua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili wakisema Kamati hiyo imefuata misingi ya Katiba ya Chama.
Msimamo wa umoja huo ni kupongeza uamuzi wa Kamati hiyo kwa uliosema ni kusimamia taasisi na mifumo ya chama, hasa katika kuhakikisha kuwa hakuna mtu aliye juu ya chama.
Hayo yalielezwa jana na Mratibu Mkuu wa Chaso, Elihuruma Himida, alipozungumza na waandishi wa habari juu ya msimamo wao kwa uamuzi uliofikiwa na CC.
"Tunasimama na chama katika uamuzi huo uliotokana na vikao halali vya kikatiba kuwavua madaraka viongozi ambao wanakwenda kinyume na Katiba ya chama chetu.
“Tunasisitiza chama kisiruhusu hata mmoja wetu kubomoa nyumba yetu hii hata kama alishiriki kuijenga, hilo haliwezekani na halivumiliki, kwani hatutabaki salama ikiwa tutaruhusu hali hii," alisema Himida.
Akizungumzia kuhusu matamko yaliyotolewa na vikundi vya wanaojiita wanafunzi wa vyuo vikuu, Himida alisema kuna baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitoa taarifa za uongo kwa kudai kuwa Chaso imetoa tamko kupinga uamuzi wa CC ya Chadema.
"Taarifa za sisi kupinga uamuzi wa CC si ya kweli, na ni upotoshaji mkubwa kwa Watanzania na ukweli wa uovu huo, ni kuwapo kikundi cha vijana waliofukuzwa ndani ya Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) mapema mwaka huu kwa makosa ya usaliti na wengine kukimbilia CCM ambao ni Mtela Mwampamba, Habib Mchange, Juliana Shonza na Greyson Nyakarungu.
"Kikundi hiki ndicho kimekuwa kikipita mitaani na kukusanya vijana wa CCM wanaojipachika uanachama wa Chadema na kujipatia vyeo vya Chaso, kisha kutoa matamko ya kupingana na uamuzi wa chama," alisema Himida.
Alisema wapo waliojitambulisha kuwa viongozi wa Chadema katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jambo ambalo halina ukweli na kudai kuwa watu hao wamepandikizwa na CCM huku wakidai kuwa na ushahidi.
Aliongeza kuwa wengine kati yao walijitambulisha kuwa viongozi wa Chaso kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, jambo ambalo alisema ni uongo kwa kuwa uongozi wa Chaso, Chuo Kikuu cha Ardhi ulisimamishwa Januari 19, kutokana na utendaji mbovu wa uongozi huo, hivyo vijana hao hawana uhalali wowote wa kufanya shughuli kwa ngazi ya uongozi au uanachama.
"Tunatambua kwa dhati kuwa Novemba 24 vijana hawa walifanya jitihada za kushawishi wanafunzi wa vyuo vikuu kuungana nao kupinga uamuzi wa CC ingawa hawakufanikiwa kufanya hivyo, tamko la Novemba 27 ilikuwa ni mwendelezo wa jitihada zile zile za awali, lakini kwa mfumo tofauti zaidi," aliongeza.
Mwenyekiti wa Chaso Tawi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mussa Ndile, alisema Chadema haijaonea mtu kwa kuwa waliochukuliwa hatua walikutwa na makosa.
Alisema Katiba ya Chama hicho imeweka wazi kuwa kiongozi au mwanachama atakayekwenda kinyume ni lazima achukuliwe hatua, hivyo uamuzi ni sahihi.
"Hatuwezi kukubaliana na mtu bila kujali ushawishi wake ndani ya chama, hata kama anakubalika hatuwezi tukaona anakwenda kinyume na tukamwacha aendelee," alisema.
Viongozi waliovuliwa uongozi pamoja na Zitto ni aliyekuwa Mjumbe wa CC, Dk Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Kutoka Arusha, habari zinasema, viongozi na wanachama wa Chadema Monduli mkoani hapa wamejitokeza kupinga uamuzi wa kuvuliwa nyadhifa zote ndani ya chama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.
Akizungumza kwa niaba ya baadhi ya wanachama aliofuatana nao jana, Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Monduli ambaye pia ni mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema, Amani Silanga alisema uamuzi wa Kamati Kuu unahitaji kupitiwa upya kabla ya utekelezaji wake.
Silanga alisema kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho bado kuna kasoro za kikatiba katika kufikia uamuzi wa Kamati Kuu, hivyo kuhitaji kupitiwa upya.
“Kwa kuwa Kamati Kuu imeshatamka uamuzi wake ambao unaonekana kukiuka baadhi ya vipengele vya Katiba, tunaomba sasa suala hilo lipelekwe kwenye Baraza Kuu la chama ambalo ni chombo cha juu ili kujadiliwa na kutolewa uamuzi,” alisema Silanga.
Alisema anaamini mahali kokote kwenye demokrasia ya kweli na uwazi, suala lolote zito hushughulikiwa kwa taratibu kupitia vyombo vyote vya juu vya uamuzi, ili kudhihirisha uhalali wa uamuzi mzito unaochukuliwa.
Alisema kiongozi kujenga mtandao ndani ya chama ili apate madaraka si kosa kubwa kama inavyotaka kuaminiwa na wala si uasi au uhaini.
“Mwanasiasa yeyote makini mwenye malengo makubwa kisiasa lazima atengeneze mtandao wa kumwezesha kufikia malengo yake kisiasa ilimradi hayaui chama,” alisema Silanga.
“Hata Marekani tumeshuhudia Obama (Rais Barack) na wenzake wakitengeneza mitandao ya kuwawezesha kupata ridhaa ya kuteuliwa na vyama kugombea urais wa nchi hiyo,” alisema.
Aidha, alisema nchini kuna mitandao mingi ya wanasiasa ya kuwawezesha kufikia malengo ya siasa na hawajapata kuitwa wahaini.
Wakati huo huo, viongozi wa vyama vyote vya siasa Arusha, jana walikubaliana kwa kauli moja kuitisha mkutano mkuu wa vyama hivyo wiki ijayo wenye lengo la kutangaza amani mkoani hapa.
Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid, wazungumzaji wakuu watakuwa viongozi wote wakuu wa vyama hivyo ambao wataruhusiwa kuvaa sare za vyama vyao na si wafuasi wala wananchi watakaokuja kusikiliza hotuba.
Maazimio hayo yalifikiwa Septemba 22 mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na kubarikiwa jana na viongozi wa dini mkoani hapa.
Akizungumzia hilo, Jaji Mutungi alisema viongozi hao waliona umuhimu wa amani Arusha kwani ni kitovu cha utalii na ina taasisi nyingi za kimataifa hivyo kutokuwa na amani ni doa kubwa.