![]() |
Kamanda Geofrey Kamwela. |
Watu wawili wamekufa katika matukio tofauti mkoani hapa, likiwamo la kikongwe kupigwa fimbo kichwani na mkwewe aliyedai kuchoka kumlea.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alimtaja aliyeuawa kuwa ni Doris Chiwiche (80) ambaye anadaiwa kushambuliwa na Egila Petro (42) mkazi wa kijiji cha Mpola wilayani Manyoni.
Alisema shambulio hilo lilitokea Novemba 18 saa nane mchana na kikongwe huyo alifariki Novemba 27.
Kamanda Kamwela alisema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa chini kwa chini kati ya Egila na mkewe huyo, ikidaiwa kuwa Egila alikuwa akimshinikiza mume wa bibi amwondoe na kumpeleka kwa ndugu zake wengine kwa vile yeye amechoka kumlea.
Katika tukio lingine, John Samson ‘Liongo’ (37) mkazi wa Misuna mjini hapa aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani na tumboni na watu wasiojulikana. Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Mnang'ana wilayani Ikungi Novemba 27, saa 6 mchana.
Kamanda Kamwela alisema uchunguzi wa awali ulionesha kuwa siku ya tukio marehemu akiwa na watu wasiojulikana, aliondoka Singida Mjini kwa gari ambalo halijafahamika na walipofika Mnang'ana waliingia porini ambako walimshambulia John.
Alisema kwenye eneo la mauaji, polisi waliokota maganda matatu ya risasi zinazotumika za bunduki aina ya SAR na SMG risasi zake zikiwa zimetumika.