Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

'NGUVU YA UMMA' YAKWAMA KUMNASUA MBUNGE WA CHADEMA JELA...

$
0
0
Salvatory Machemli.
Utaratibu wa Chadema kutumia kinachoitwa ‘nguvu ya umma na vurugu’ kushinikiza sheria ipindishwe kwa maslahi yake, umekwama kumnusuru Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli anayetumikia adhabu ya kukaa jela kwa siku 14.

Jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini  ya Chadema, Sylvester Masinde, alikiri kuwa nguvu ya umma iliyodaiwa kutumika kumnusuru Machemli, ni upotoshaji na hali ilivyokuwa, mamlaka zilishajiandaa  kukabiliana nao.
Kutokana na hali halisi, Masinde alisema chama hicho hakiwezi na wala hakina  mpango wa kutumia nguvu  ya umma,  kushinikiza  Machemli atoke mahabusu.
Masinde alifikia hatua ya kuwambia  viongozi wa ngazi ya msingi wa chama hicho kuwa  ni vema utaratibu uliowekwa kisheria uheshimiwe.
Kiongozi huyo ambaye  pia ni mjumbe wa  Kamati Kuu   ya chama hicho, alisema suala  hilo limechunguzwa na kubaini ni kweli Machemli aliruka dhamana,  hivyo  Mahakama Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka  ya kutengua  uamuzi huo.
Machemli anakabiliwa na kesi ya uchochezi na Novemba  6 aliamriwa na Mahakama  ya Wilaya kwenda rumande kwa  siku 14, baada ya kuidharau   kwa kutotokea wakati kesi ikiitwa.
Tofauti na ilivyokuwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye alisema lupango ndiko kwenye wapiga kura wake, kwa Machemli Chadema imeamua kufuata utaratibu kumtoa.
Kabla ya kuahirisha kesi hiyo, Hakimu Mkazi
Mfawidhi  wa Mahakama  hiyo, Faustine Kishenyi aliagiza mbunge huyo baada ya siku 14 afikishwe tena mahakamani hapo  akiwa na  wadhamini wengine watatu  ambao kila mmoja atatakiwa kuwa na hati  ya nyumba.
Katika hatua  nyingine,  kiongozi huyo wa  ngazi ya  juu wa Chadema  alikiri kuwa mamlaka wilayani humo, zilishajiandaa kukabiliana na nguvu ya umma.
Alidai alifuatana  na viongozi  wengine wa chama hicho kwenda kumjulia hali mbunge huyo, lakini barabarani walikuwa wakifuatwa kwa karibu na gari la Polisi.
Hata hivyo, walipofika gerezani,  walitakiwa na Mkuu wa Gereza waondoke.
Akizungumzia sababu za kuzuiwa  kuingia gerezani hapo, kiongozi huyo alidai anahisi pengine mamlaka husika zilitishwa na uvumi usio wa kweli kuwa  zingetumika  nguvu za umma  kushinikiza Mahakama  itoe dhamana kwa mbunge huyo.
Hata hivyo, Mkuu wa Magereza  wa Wilaya, Edward   Nyabange, alisema viongozi hao wa Chadema wakiwa zaidi ya  10  walizuiwa  kuingia  gerezani hapo kwa sababu ya kutofuata utaratibu.
Alisema   utaratibu  uliopo  unaelekeza Jumapili  pekee ndiyo  mahabusu na wafungwa wanaruhusiwa kutembelewa na jamaa zao na kuongeza kuwa mbali na viongozi hao kuvunja utaratibu, pia  idadi
yao  ilikuwa kubwa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles