Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

JAPAN YATOA FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA ZA JUU MAENEO YA UBUNGO NA TAZARA...

$
0
0
Msongamano wa magari eneo la Ubungo.
Serikali ya Japan, imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara maeneo ya Tazara  na Ubungo.

Mkurugenzi wa Miradi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Chrispians Ako, alisema hayo jana, wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa utekelezaji wa miradi ya maji Tabora, pamoja na uendelezaji wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara ya Kilwa hadi Kamata.
Barabara hizo za juu ni sehemu ya barabara za aina hiyo sita zinazotarajiwa kujengwa Dar es Salaam, ili kukabiliana na msongamano.
Maeneo mengine yenye makutano ya barabara kutakakojengwa  barabara za juu ni Magomeni, Faya, Kamata na Chang'ombe.
Barabara hizo pia zinatarajia kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kutoa unafuu wa magari yanayotoa mizigo katika bandari hiyo, kwenda nchi zisizo na bahari.
Ingawa Ako hakufafanua kuhusu kiasi cha fedha kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi huo, lakini taarifa za Tanroads zinaonesha kuwa ujenzi wa barabara ya Tazara-Ubungo, ndio unaotarajiwa kuanza na gharama zake ni Sh bilioni 52.2.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Serikali ya Japan ilishatoa Sh bilioni 1.1 kwa ajili ya upembuzi yakinifu uliotarajiwa kukamilika tangu Julai.
Aidha, Serikali kwa maelezo ya taarifa hizo, imetenga Sh bilioni 28.6 katika bajeti ya mwaka huu, kwa ajili ya kukabiliana na foleni katika Jiji hilo.
Fedha hizo zinatarajiwa kutumika kuboresha barabara zinazosaidia kupunguza foleni ambapo Sh bilioni moja, itatumika kama mchango wa Serikali katika ujenzi wa barabara ya juu Tazara.
Mbali na fedha hizo ambazo zimeshatolewa, jana  Serikali ya Japan ilitoa Sh bilioni 30.6 za utekelezaji wa miradi ya maji Tabora, pamoja na uendelezaji wa awamu ya pili ya ujenzi wa barabara ya Kilwa-Kamata.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa utekelezaji wa miradi hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Servacius Likwelile, alisema kati ya fedha hizo, Sh bilioni 28.95 zitatumika kwa miradi ya maji mkoani Tabora.
ÒNapenda kuchukua fursa hii kuishukuru Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), kwa msaada huu ambao utasaidia kutatua matatizo ya majisafi hasa vijijini,Ó alisema Likwelile.
Alisema mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo, yatachangia maendeleo ya nchi kwa kuwa upatikanaji maji katika maeneo hayo hasa vijijini, utapunguza muda mrefu unaotumika kutafuta maji na kutoa fursa kwa wakazi wa maeneo hayo kufanya shughuli za maendeleo.
Alisema Serikali ya Tanzania imejizatiti kutimiza Malengo ya Milenia (MDGs) kwa kupunguza angalau nusu ya Watanzania ambao hawapati maji safi na salama.
Ofisa Ubalozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsunaga, alisema Serikali ya Japan imekuwa ikifurahia na kujivunia ushirikiano wake wa takribani miaka 50 na Tanzania, na imejizatiti kuhakikisha ushirikiano huo unadumu kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bashir Mrindoko, alisema Japan ni mshirika wa muda mrefu katika sekta ya maji nchini na msaada huo wa Tabora, utasaidia utekelezaji wa Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

Trending Articles