Jamaa mmoja alikuwa akimpiga mkewe asubuhi na mapema katika moja ya mitaa ya Mwananyamala. Wakati akimpa kichapo mkewe, jamaa alikuwa akimtuhumu kwa utovu wa nidhamu na dharau katika ndoa yao. Wakati akiendelea kumtandika huku mke akipiga kelele za kuomba msaada, akatokea jirani mmojawapo na kumsihi yule mume kwa kitendo chake na mambo yakawa hivi.
Jirani: "Bwana Tito usifanye hivyo, mke huwaga hapigwi. Dawa yake huyo kumuolea mke wa pili!" Ghafla yule mke akanyamaza kulia na kujibu: "Hasidi mkubwa wewe. Tena potea kabisa hapa, hayakuhusu haya. Mume wangu tafadhali endelea kunipiga maana tabia yangu mbaya sana siku hizi!!" Duh, mume akabaki mdomo wazi asijue la kufanya...