Watu wasiojulikana wamehujumu mawasiliano ya Ikulu ndogo Arusha baada ya kuiba nyanya za simu
za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) mkoani humo.
Wizi huo unadaiwa kusababishia kampuni hiyo hasara ya zaidi ya Sh 1,002,108,083.10. Wizi huo ulifanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu Januari hadi Desemba 2012.
Meneja wa TTCL mkoani Arusha, Laibu Leonard alikiri kuwepo na hujuma hiyo, iliyofanywa na kundi la watu wasiojulikana. Wizi huo licha ya kuathiri Ikulu ndogo, pia umeathiri maeneo mengine mkoani Arusha.
Laibu alieleza wizi huo umesababisha kampuni iingie hasara, kwa kulazimika kurejesha upya mawasiliano ya simu katika eneo hilo la Ikulu ndogo.
Alifafanua kwamba shirika limepoteza mapato ya zaidi ya Sh 951,039,860 kutokana na hujuma hizo, fedha ambazo Shirika lingekusanya kutoka kwa wateja wake.
Kwa mujibu wa Laibu, wateja zaidi ya 2,274 waliathirika na matukio zaidi ya 41 ya wizi huo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha.
Maeneo mengine yaliyoathirika na wizi huo ni barabara ya Kenyata, Kwa Iddi, Sakina, Njiro na Sanawari. Mengine ni Chuo cha Ufundi, Esso, Themi, Sekei, Barabara ya Moshi, Mianzini na Soweto.
Katika maeneo ya Mianzini wateja zaidi ya 853 waliathirika, Esso wateja 453, Njiro wateja 338 na Themi wateja zaidi ya 171.
Meneja huyo alitaka wananchi kushirikiana na TTCL, kutoa taarifa za watu wanaojaribu kuhujumu mawasiliano ya simu.