Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all 4100 articles
Browse latest View live

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AUAWA KWA KUDAIWA MWIZI

$
0
0


Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini hapa, Helma Michael (22)  ameuawa kwa kupigwa mawe na wanafunzi wenzake, wakimhisi kuwa ni mwizi wa kompyuta ndogo za mkononi na deki chuoni hapo. 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Valentino Mlowola, alisema jana kuwa mwanafunzi huyo aliuawa Mei 13 mwaka huu saa 4.00 usiku, katika eneo la Nyamalango Malimbe, ambapo baada ya kubainika katika eneo hilo alianza kupigwa kwa mawe, fimbo na mapanga hadi kusababisha kifo chake.
“Huyu ameuawa katika tuhuma ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa,” alisema.  
Kutokana na mauaji hayo, watu 17 wamekamatwa na Polisi  imeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo huku Kamanda Mlowola akiwataka watu kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu ambao hawana hatia.
Katika tukiojingine, Kamanda Mlowola alisema mkazi wa Kijiji cha Bugula Kata ya Bwiro wilayani Ukerewe, Bazil Amran aliuawa kwa kupigwa na kipande cha ubao kichwani na Parapara Paulo (36)  kwa tuhuma za wizi. 
Kwa mujibu wa Kamanda Mlowola, mauaji hayo yalitokea Mei 12mwaka huu saa 11 alfajiri  kijijini hapo ambapo alisema mtuhumiwa amekamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.
Aidha katika tukio jingine, Kamanda Mlowola alisema Mei 13 mwaka huu majira ya saa saba mchana katika eneo la Mkuyuni kata ya Mahina wilayani Nyamagana, askari polisi waliokuwa doria waliwakamata Sylvesta Musa (31) na Noela Joseph (34) wote wakiwa ni wakazi wa Mkuyuni wakiwa na bastola aina ya LOCK NO. TZ CAR 91968 ikiwa na risasi tano kwenye magazinie yake.


HUYU NDIYE KINARA WA WIZI KWENYE MABENKI

$
0
0

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kubaini mtuhumiwa kinara wa wizi wa mabenki, Ronald Mollel (37), ambaye ni mume wa Meneja wa Benki ya Barclays tawi la Kinondoni, Alune Kasililika, anayeshikiliwa na jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova (pichani), alitoa madai hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio ya ujambazi.
Alisema Mollel  ni  makazi wa Kimara Bonyokwa na taarifa za kuaminika zinadai amekuwa akipanga njama na kushiriki kikamilifu matukio mbalimbali ya uhalifu na kupora mabenki.
Alidai mtuhumiwa huyo ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi  ya benki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika benki hizo.
‘’Jeshi la Polisi tumeamua kuweka picha ya  mtuhumiwa huyo hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi shirikishi, ili akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi,’’ alisema Kova.
Pia alisema wamekamata watu watatu kwa tuhuma za ujambazi wakiwa na silaha mbili aina ya Shotgun na risasi 12, Rediocall na sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Isihaka Salehe, Alex Andrew na Odinga Swalehe  ambao walikamatwa maeneo ya Chamanzi katika Mkoa wa Kipolisi wa Temeke.
Pia alisema jeshi hilo, limefanikiwa kuufumua mtandao unaojihusisha na ujambazi jijini Dar es Salaam, ikiwemo uvunjaji na kupora nyumba za ibada.
Alisema operesheni hiyo ilianza April 29 mwaka huu, walikamata majambazi sugu wawili nao wakawataja wenzao 13.
‘’Watuhumiwa waliokamatwa katika mtandao mzima ni Shaban Mafuru (36), mkazi wa Magomeni, Abdallah Hussein (52) mkazi wa Tabata Mawenzi, walikutwa kwenye gari namba T259ADB,  ’’ alisema.
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na meno 25 ya kiboko na mmoja akiwa na vipande nane vya meno ya tembo.

BASI LAJIBAMIZA KWENYE LORI NA KUUA WATU 10 MWANZA

$
0
0


Watu 10 wamekufa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria walilokuwa wakisafiria kugonga lori lililokuwa na kokoto  lililoegeshwa kando ya barabara kasha kupinduka katika eneo la Nyamhongholo, jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, Daktari wa Idara ya Dharura, Dk Regina Mutayangulwa, alisema miili ya abiria hao na majeruhi   ilipokewa hospitalini hapo juzi usiku.
Majeruhi waliolazwa katika wodi za upasuaji ni pamoja na wanawake watatu waliolazwa katika wodi namba 9C na wanaume saba waliolazwa katika wodi namba 6Cna 8E na hali zao zinaendelea vizuri.
Waliojeruhiwa ni pamoja na Verynice Protas (22), Rosemary Petro (26), Prisca Peter (25), Hamad Haruna (22) ambaye amevunjika mkono wa kushoto na paji la uso kuharibika na Benson Joseph (27).
Wengine ni Nyanda Sahani, Magesa Musa (30), Rushinge Nyerere, Japhet Mlangwa (23) na Shija Nyanda Ngwenda.
Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentine Mlowola, alisema ilitokea Mei 13 saa moja usiku katika Barabara Kuu ya Mwanza- Musoma.
Alisema ajali hiyo ilihusisha gari lenye usajili namba T 769 CQE aina ya Toyota Coaster, lililokuwa likiendeshwa na Yohana Mayandakia likitokea Mwanza kwenda Bunda, ambapo liligonga namba Lori aina ya Iveco, lenye namba T832 AEF  na tela namba T 187 AEF.
Alisema lori hilo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara na dereva aliyeitwa Emmanuel Zakaria (33) ambalo lilikuwa bovu.
Kamanda Mlowola alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kutokuwa mwangalifu na ishara iliyokuwa imewekwa mbele ya gari lililokuwa bovu. Dereva wa lori anashikiliwa Polisi kwa uchunguzi zaidi.

KUMBE 1X3 NI SAWA NA 3X1

$
0
0


Mwanafunzi mdadisi kambana mwalimu wake wa Hisabati kwenye kona na mambo yakawa hivi. MWANAFUNZI: Mwalimu, umesema 3X1 ni sawa na 1X3? MWALIMU: Haswaa, umenielewa vizuri kabisa. MWANAFUNZI: Kwahiyo basi nikibadili dozi ya malaria iliyoandikwa 1X3 badala yake ninywe 3X1 ni sawa tu!! Kasheshe…

Article 3

$
0
0
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa huduma ya M-PAWA ya kampuni ya Vodacom wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais Jakaya Kikwete katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam jana.

Article 2

$
0
0
Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee akionesha begi lenye Bajeti ya Serikali ya Zanzibar kwa mwaka 2014/2015 jana.

Article 1

$
0
0
Sehemu iliyojengwa na wezi wa maji kama Kituo cha Kusambaza Maji (Pumping Station) kwa wateja waliofanya maungio kinyume cha utaratibu eneo la Kimara Michungwani.

Article 0

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO), Raymond Benjamin (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana.


MGOGORO ZIWA NYASA WASUBIRI UCHAGUZI MKUU WA MALAWI

$
0
0


Jopo la marais wa zamani wanaoshughulikia mgogoro wa Ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi, linasaubiri kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa Malawi unaotarajia kufanyika Jumanne ijayo, ili kuingia katika awamu ya pili ya mazungumzo ya kumaliza mgogoro huo.
Hayo yalisemwa juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe, kufuatia swali la mwandishi mmoja wa Malawi aliyetaka kujua msimamo wa sasa wa Tanzania kuhusu mgogoro huo.
Waziri Membe alikuwa jijini Blantyre, Malawi, akiongoza ujumbe wa Tanzania uliosafirisha mwili wa aliyekuwa balozi wa nchi hiyo nchini Tanzania, Flossie Gomile-Chidyaonga, aliyefariki ghafla jijiji Dar es Salaam ijumaa iliopita. Mwili huo ulisafirishwa kwa ndege ya serikali ilyotolewa na Rais Jakaya Kikwete, jambo ambalo limewakuna wananchi wa Malawi wakiipongeza hatua hiyo.
"Kama wote mnavyojua, Tanzania na Malawi zilimua kupeleka suala hili kwenye jopo linaloongozwa na Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim  Chisano, akisaidiwa na Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki na Rais wa Mstaafu wa Botswa, Festus Mogae. 
"Tulichukua uamuzi huu kutokana na uhusiano mzuri wa kindugu ambao nchi zetu, Tanzania na Malawi, tunao, kwamba badala ya kubishana sisi wenyewe kwa wenyewe tukipe chombo kingine kutazama mgogoro wenyewe na kutoa uamuzi," alisema.
Alisema kwa kuwa Malawi inafanya uchaguzi wake mkuu, jopo la marais hawa wa zamani liliona lisubiri uchaguzi huo kumalizika. Alisema baada uchaguzi, serikali itakayoingia madarakani, iwe ya sasa inayoongozwa na Rais Joyce Banda ama ya sura nyingine, basi suala hilo litazungumzwa tena katika awamu ya pili.
"Ni matumaini yetu kwamba jopo la wazee wetu hawa kwa kushirikiana na wanasheria waliobobea, watatupeleka sehemu ambayo tutajua namna nzuri ya kulimaliza suala hili na tuna imani kwamba sisi kama ndugu ambao tumekuwa tukilitumia ziwa hili karne kwa karne suala hili litapata ufumbuzi mzuri," alisema.
Alisema kwa sasa mtazamo wa Tanzania umejikita kwenye maana ya "mpaka baina ya nchi na nchi unaotokana na ziwa (mto ama bahari)."
"Hata mki-google (mkitumia injini ya google ya kutafutia habari kwenye mtandao) mtaona kwamba uamuzi wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika eneo hili bado haujawahi kufikiwa. Kwa vile hayajawahi kuwepo mazungumzo ya kujadili mpaka uweje, kinachotakiwa, kwa mantiki hiyo, ni nchi hizi kuunda tume za mpaka kwa pamoja, kuangalia na kisha kukubaliana ni wapi mpaka kwenye ziwa hili uwe, kama ni katikati ama vinginevyo katika namna ambayo inakubaliwa kimataifa," alisema.
Mgogoro wa ziwa Nyasa ambao hata hivyo ulikuzwa sana na vyombo vya habari kuliko hali halisi, ulikuja baada ya Malawi kudai kwamba ziwa hilo lote liko nchini Malawi na kwamba mpaka ni ufukweni kwa upande wa Tanzania.
Dai hili lilileta mtazamo kwamba kwa upande wa Tanzania, mpaka ni pale yanapoanzia maji ya Ziwa Nyasa na hivyo Mtanzania anapovua samaki ama kuteka maji kwenye ziwa hilo, anakuwa ameingia nchi nyingine ya Malawi.

RAIS KIKWETE ABEBESHA WAKUU WA MIKOA MZIGO

$
0
0


Rais Jakaya Kikwete, amewaagiza wakuu wa mikoa kupunguza vifo vya watoto na akina mama vinavyotokana na uzazi katika mikoa yao, huku akiwahadharisha kwamba atafuatilia kwa karibu utendaji wao kuona namna wanavyoshughughulikia tatizo hilo.
Alionya kuwa hatakuwa na huruma na Mkuu wa Mkoa,  atakayeshindwa kuweka mikakati ya kupunguza tatizo hilo katika mkoa wake, na akawataka waachane na kisingizio cha ufinyu wa bajeti ambacho kimekuwa  kichaka cha viongozi wasiowajibika.
Akizundua mpango mkakati wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na  vya watoto wachanga na wale wa chini ya miaka mitano, Rais Kikwete alisema kuanzia sasa jambo la kwanza atakalofuatilia katika utendaji wa wakuu wa mikoa, ni namna wanavyoshiriki kupunguza vifo vya watoto na akina mama katika maeneo yao.
"Mimi sio kiongozi wa kusikiliza na kuamini ninayoambiwa, hili linanigusa kwa karibu… nawaambia nitafuatilia utendaji wenu kwa karibu, lengo nataka vifo vya watoto wachanga na wale wa chini ya miaka mitano pamoja mama wajawazito vinapungua," alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema wakuu wa mikoa, wamekuwa hawafuatilii masuala ya afya hadi litokee tatizo la dharura la kipindupindu, wakati vifo vya watoto na akina mama wanaokufa kwa uzazi vinaongezeka hata kuliko wanaokufa kwa kipindupindu.
Aliwataka suala hilo iwe ajenda ya kisiasa katika ngazi zote za Serikali na akawaagiza wakuu hao wa mikoa, wanaporejea mikoani kwao wakasambaze maagizo hayo katika ngazi za chini yao, ili utekelezaji uanze mara moja.
"Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wanafikiri suala hili ni la waganga wakuu na watumishi wa afya, hata hawaulizi hali zikoje mikoani kwao, sasa lichukulieni hili kuwa la dharura...nikija huko jambo la kwanza kuuliza na kufuatilia ni suala hili," alisema Rais Kikwete.
Aliwataka wakuu hao wa mikoa kuweka mikakati ya kupunguza tatizo hilo na yeye akaahidi kuwa atalifuatilia binafsi utendaji wa kila Mkuu wa Mkoa, kupitia kadi maalum za kutolea taarifa za vifo vya watoto wachanga, watoto wa chini ya miaka mitano na akina mama wanaokufa kwa matatizo ya uzazi.
Alisema baadhi ya vifo vya watoto na wajawazito vinatokea kwa sababu ya uzembe wa watumishi wa afya, na akaeleza kuwa suala hilo linawezekana iwapo tu viongozi watatimiza wajibu wao kwa kufuatilia kwa karibu.
"Kipimo cha uwajibikaji wenu, itakuwa kupitia kadi hii," alisema Rais Kikwete na kuahidi kuwa atahitaji kupokea taarifa ya kila mkoa kila baada ya miezi minne, kuona namna wakuu wa mikoa na watendaji wao wanavyoshughulika na tatizo hilo.
Rais Kikwete alisema sekta ya afya kwa sasa haiko katika mpango wa matokeo makubwa sasa, ameagiza kitengo cha Rais cha kufuatilia utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), waiweke sekta hiyo kwenye mpango huo.
Rais pia alitoa mwito kwa wajawazito, kuhakikisha wanapata chakula bora chenye lishe, ili kuongeza usalama wakati wanapoenda kujifungua. Alisema pia  familia zinatakiwa kuzingatia uzazi wa mpango, ili kuwalea watoto na kuwapa mahitaji yao ya msingi.
Awali akitoa tamko la wakuu wa mikoa, ambalo waliazimia juzi baada ya kufanyiwa semina, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christin Ishengoma, alisema wameazimia  kila mkoa uandae mpango mkakati wa kupunguza tatizo hilo ambao unatekelezeka na uwe shirikishi.
Alisema kuanzia sasa kila mkoa utawatambua wajawazito wote walioko katika maeneo yao na watoto wa chini ya miaka mitano, ili  kuwafuatilia kwa karibu na kuwapatia huduma za msingi zinazotakiwa.
Akitoa hali halisi ya vifo vya watoto na wajawazito wanaokufa kwa uzazi, Dk Neema Rusibamanyika, alisema akina mama 7,900 wanakufa kila mwaka kwa matatizo ya uzazi na vichanga 40,000 katika kila vizazi 100,000 pia hufariki.
Sababu za vifo vya watoto, alisema ni kuugua nimonia, magonjwa ya kuharisha na Malaria, wakati vifo vya wajawazito husababishwa na ukosefu wa vifaa tiba, upungugu wa watumishi, miundombinu mibovu na ucheleweshaji wa huduma.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa asilimia 51 ya wajawazito ndio wanaojifungulia hospitalini, wakati asilimia 49 hujifungulia kwa wakunga wa jadi. 
Hali hiyo ni chini ya Malengo ya Millenia, yanataka ifikapo mwaka 2015 asilimia 80 ya wajawazito wawe wanajifungulia hospitalini.

KITENDAWILI CHA USAFIRI TRENI YA TAZARA BADO KUTEGULIWA

$
0
0


Abiria wa treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), ambayo inatakiwa kuondoka leo kwenda Zambia, wako njia panda kutokana na wafanyakazi wa shirika hilo kuendelea na mgomo wakidai mishahara yao.
Wakati mgomo huo ukiendelea, leo treni ya abiria kwa mujibu wa ratiba ya shirika hilo inatarajiwa kusafiri, hali inayotia wasiwasi kuwa huenda abiria watakwama stesheni, kwasababu hawajarudishiwa fedha zao kama walivyorudishiwa abiria wa treni iliyotarajiwa kuondoka Jumanne ya Mei 13 mwaka huu. 
Wafanyakazi wa Tazara jana waliendelea kukusanyika katika viwanja vya Tazara, wakisubiri uamuzi wa Menejimenti ya shirika hilo kuhusu malipo yao, ndipo waendelee na kazi hata hivyo hakujitokeza kiongozi yeyote katika Menejimenti kuzungumza nao.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli nchini (Trawu) Kanda, Yusuph Mandari aliwataka wafanyakazi wenzake kuwa na uvumilivu katika kipindi hicho wakati wakisubiri kikao kitakachofanyika leo cha Bodi ya Wakurugenzi wa Tazara kutafutia ufumbuzi tatizo lao kama walivyoahidiwa na Mkurugenzi Mkuu wao Phiri.

WEREMA AOMBA RADHI KWA KAULI YAKE YA KIBAGUZI

$
0
0


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, jana aliomba radhi Bunge baada ya kutoa kauli, iliyoonesha ubaguzi kwa wabunge kutoka Zanzibar.
Kabla ya kuomba radhi, kauli hiyo ilisababisha wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), kutoka nje ya Bunge  kuonesha kukerwa na kauli hiyo.
Muda mfupi baadae, wabunge hao waliungwa mkono na wabunge kutoka Bara, ambao wanatoka  Chadema na NCCR Mageuzi, ambao nao walitoka na kuwaacha wabunge wa CCM na mbunge wa UDP, John Cheyo.
Awali kabla ya kutoka nje, Mbunge wa Ole, Rajabu Mbarouk (CUF), aliomba muongozo wa Spika akilalamikia kauli ya Werema wakati akimjibu Mbunge wa Mkanyageni, Habibu Mnyaa (CUF).
Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na sio katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa sio kila kitu kitaulizwa ndani ya bunge hilo. 
Hoja ilianzia kwa Mnyaa, wakati akiomba Kamati ya Matumizi ya Bunge  iliyokaa kupitisha vifungu vya hotuba Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2014/15. 
Mbunge huyo aliituhumu Wizara ya Katiba na Sheria kuwa ni moja ya Wizara muhimu lakini imekuwa ikivunja sheria na haki za binadamu. 
Baada ya hoja hiyo, Werema alijibu: “Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa sio mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu.”
Mara baada ya bunge kurejea, Mbunge wa Ole, Rajabu Mbarouk (CUF), aliomba mwongozo wa Spika akitaka ufafanuzi wa kauli hiyo kwamba ilikuwa ya ubaguzi. 
“Mheshimiwa Spika, wakati wa majadiliano na wakati ambapo Mheshimiwa Mnyaa anaongea na kutaka ufafanuzi wa haki za binadamu, huu ni ubaguzi na haupaswi kufanywa na mtu msomi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” alisema Mbarouk. 
Hata hivyo Spika alipinga na kusema; “hakuna mwongozo wowote kwa kuwa hata wewe umevunja sheria kwani hata nilipokuambia kaa chini, umeendelea kuzungumza, tunaendelea Katibu.” 
Baada ya kauli ya spika, wabunge wa Zanzibar walihamasishana na kuamua kutoka nje wote kwa wakati mmoja na kuwaacha wabunge wenzao wa upinzani wakiendelea kuitana na kutafakari cha kufanya.
Spika alifafanua kuwa Mbarouk alikosea kumshutumua Spika hadharani, kwa kuwa kanuni zinaelekeza kama amekosea, malalamiko yapelekwe katika Kamati ya Kanuni. 

SERIKALI YASEMA UDA NI 'MALI YA UMMA'

$
0
0


Hadi sasa mmiliki halali wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali kupitia Msajili wa Hazina.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima alisema hayo jana bungeni na kuongeza kuwa Serikali iliondoa kesi mahakamani ya watuhumiwa wa UDA, ili kuruhusu uchunguzi kufanyika upya.
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), Mdee alitaka kauli ya Serikali kuhusu utata wa utaratibu uliotumika katika uuzwaji wa hisa za Serikali katika Shirika hilo.
Pia alitaka kujua nani mmiliki halali wa hisa hizo kwa sasa pamoja na mgawanyo wa hisa kwa wamiliki hao.
Malima alisema hisa ndani ya Shirika la UDA hazijauzwa, mgawanyo wa hisa halali ni kama ulivyosajiliwa kwa msajili wa makampuni, kwa maana ya Halmashauri ya Jiji asilimia 51 na Serikali kupitia Msajili wa Hazina asilimia 49.
Naibu Waziri alisema mwaka 2006 Serikali iliamua kuuza hisa zake kwa asilimia 49 ili kupata mwekezaji mahiri mwenye uwezo wa kuliboresha shirika hilo.
Hata hivyo alisema Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Sekta ya Umma  (PSRC) ilishindwa kumpata mwekezaji aliyekidhi vigezo vilivyowekwa.
Januari 2010 kwa mujibu wa Malima, Bodi ya UDA iliiarifu Serikali kuwa amepatikana mwekezaji ambaye ni Kampuni ya Simon Group ambayo ingeuziwa hisa za Serikali pamoja na hisa 7,880,303 ambazo hazikugawiwa wakati UDA inaanzishwa.
Malima alisema Serikali iliagiza Bodi kusitisha mpango wa kuizuia Simon Group Limited hisa zozote kutokana na kukiukwa kwa taratibu na misingi ya Sheria.
Akiuliza swali la nyongeza, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu kampuni hiyo kuendelea kumiliki na kuendesha Kampuni ya UDA sasa.
Mbunge huyo alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alishafanya uchunguzi kuhusu uuzwaji wa hisa za UDA na kubaini  kuwepo kwa ufisadi.
Alisema ripoti hiyo iliwasilishwa kwa Waziri Mkuu Machi 30 mwaka 2011, ambapo ilibaini ufisadi wa kutisha na kutaka Serikali itoe kauli baada ya kubaini ufisadi huo.
Aidha Mnyika aligusia kitendo cha Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP), kuwasilisha hati mahakamani kutaka watuhumiwa wote wa UDA waachiwe kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.
Mnyika alisema bila majibu watazidi kuamini kama Serikali ya CCM inawalinda vigogo ambao ni mafisadi.
Akijibu hoja ya Mnyika, Malima alikiri kuwepo kwa utata kwa mazingira ya uuzwaji wa UDA kutoka pande zote mbili za umiliki yaani Serikali na Halmashauri ya Jiji. 
Alisema baada ya CAG kutoa ripoti yake ilielezea ukiukwaji   wa taratibu na sheria za uuzwaji, ndipo DPP aliamua kuondoa kesi mahakamani ili uchunguzi uendelee.
Malima alisema sasa vyombo vya uchunguzi ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) vinaendelea na uchunguzi dhidi ya ufisadi uliobainishwa na CAG.

SPIKA MAKINDA AMPASHA NYALANDU WIZARA ITAMSHINDA

$
0
0


Spika wa Bunge, Anne Makinda ameshauri Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  kuwa kitu kimoja na watendaji wake vinginevyo, wizara itamshinda.  
Ushauri huo aliutoa baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15; bila upinzani mkubwa tofauti na ilivyozoeleka.   
Katika mwaka wa fedha 2013/14, Wizara ya Maliasili na Utalii iliidhinishiwa na Bunge Sh bilioni 83.1. Kati ya hizo, Sh bilioni  68.9 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 14.1  kwa ajili ya miradi ya maendeleo.  
Makinda alisema tangu ameingia bungeni, wizara hiyo ni tete. “Tangu nimeingia bunge hili wizara hii ni tete. Mimi nilitegemea Nyalandu utafanya mabadiliko na nategemea utafanikiwa,” alisema.  
“Nendeni mkafanye  kazi kwa mujibu wa sheria na sisi tunategemea utalii ni sehemu yetu ambayo nchi inaweza kuishi vizuri zaidi bila kuleta vineno neno,” aliwaambia watendaji wa wizara hiyo wazidi kushirikiana kwani suala hilo ni la kitaifa si suala la mtu binafsi.  
Wakati wa kujadili bajeti ya wizara baadhi ya wabunge, ikiwemo Kambi Rasmi ya Upinzani, walieleza kusikitishwa kile walichosema ni mvutano baina ya Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii.  
“Hali hiyo inaonesha kuwa kuna mgongano aidha wa kimaslahi…Waziri na Katibu Mkuu wa wizara moja wanafanya kazi bila kushirikiana na kila mmoja akionekana kumvizia mwenzake hadharani, badala ya kukaa kwa pamoja kutekeleza maazimio ya Bunge,” alisema Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa wizara hiyo, Mchungaji Peter Msigwa. 

Article 6

$
0
0
Warembo wanaoshiriki Shindano la Miss Dar City Center 2014 wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana.


Article 5

$
0
0
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakimsikiliza kwa makini mkufunzi, Peter Ssali (hayupo pichani) katika mafunzi ya siku tatu kuhusu utoaji huduma bora kwa Bodi hiyo ili kuwa sambamba na bodi za vyakula Afrika Mashariki jana.

Article 4

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stellah Manyanya akizungumza na watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Uyole iliyopo mkonia Mbeya walipomtembelea ofisini kwake jana kutambulisha mpango wa SARD unaodhaminiwa na Benki ya Maendeleo Afrika (ADB).

Article 3

$
0
0
Baadhi ya washiriki wa tamasha la "Mtu Kwao" wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha jana.

ETO’O SLAMS ‘FOOL’ MOURINHO OVER AGE JIBE

$
0
0


Samuel Eto'o has described Chelsea manager Jose Mourinho as a "fool" for questioning his age and vowed to play on at the highest level for some time to come.

Mourinho, who was also Eto'o's manager at Inter Milan, was caught on camera making unguarded comments suggesting the Cameroon striker was older than his official age earlier this season.
The 33-year-old, in line to feature in his fourth World Cup this summer, responded by celebrating his next Chelsea goal as if he was a geriatric.
Now Eto'o, who is out of contract this summer after scoring 12 Chelsea goals, plans to continue to ply his trade in one of Europe's top leagues.
Eto'o told africanfootball.com: "Thanks for informing me that it will be my last World Cup.
"Today, I am 33-years-old. And it is not because a fool called me an old man that you must believe it.
"And you may have noticed that the old man was better than the youngsters.
"Some believe I am going to retire in the United States or in the Middle East, but I have regained the joy of the Champions League and I am going to carry on playing in the Champions League. Where? I am not going to tell you," he added.
"But I am going to carry on playing because physically and mentally I feel great.
"So I am going to go to this World Cup and to the next one when I will be 37.
"Some did it at 42, so I can still play in two more World Cups."
Following Chelsea's final game of the season at Cardiff, Mourinho suggested Eto'o would depart this summer, at the end of his one-season deal.
The Chelsea boss will wait until pre-season before determining the futures of his loan stars.
Mourinho presented his end-of-season report to the Chelsea hierarchy on Monday, detailing his thoughts on all matters relating to the first-team squad.
Definitive decisions on goalkeeper Thibaut Courtois, striker Romelu Lukaku and the others who spent time away from Chelsea this season will wait until after training resumes on July 8.
Courtois has impressed in his third consecutive season on loan at Atletico Madrid, helping the Spaniards to the May 24 Champions League final at the expense of his parent club, and could put pressure on Petr Cech as Chelsea number one.
Lukaku spent a second straight season on loan in the Premier League, scoring 17 goals for Everton - a tally greater than any of the strikers who remained at Stamford Bridge.
Others will also be looked at closely by Mourinho, including Victor Moses, who spent the season at Liverpool, and Marko Marin, who helped Sevilla to win the Europa League.
After Chelsea's final home game of the season, Mourinho insisted there was no rush to make decisions relating to his squad.
Tellingly, though, captain John Terry signed a one-year contract extension 24 hours after Mourinho's report was submitted.
The fates of record goalscorer Frank Lampard and left-back Ashley Cole are still to be clarified, with their contracts expiring imminently.

BAJETI YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

$
0
0

HOTUBA YA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LAKUJENGA TAIFA
MHE. Dkt. HUSSEIN ALI MWINYI (MB) AKIWASILISHA BUNGENI
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI
YA FEDHA KWA MWAKA  2014/15

UTANGULIZI

1.    Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Ulinzi na Usalama, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.

2.    Mheshimiwa Spika,kabla ya kuwasilisha hoja yangu, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, aliyenijalia kuwa na uzima na afya njema na kuniwezesha kuwasilisha hotuba yangu ya bajeti kwa mwaka 2014/15. Aidha, namshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, wa majeshi shupavu ya Tanzania, Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kuniteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mara ya pili. Ahadi yangu kwake  Mheshimiwa Rais, kwenu Waheshimiwa Wabunge na kwa Watanzania wenzangu, hususan wenye mapenzi mema na nchi yetu, yenye amani, utulivu, upendo na mshikamano ni  kwamba, nitatumia uwezo na nguvu zangu zote kutekeleza majukumu mazito na nyeti mliyonikabidhi kwa umakini mkubwa, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu.

3.    Mheshimiwa Spika,napenda pia kuwashukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Kayanza Pinda (Mb) kwa miongozo, ushauri na ushirikiano mkubwa wanaonipatia katika kutekeleza majukumu ya Wizara yangu.  Vilevile, nakushukuru wewe Mheshimiwa Spika na Kamati yako Tukufu ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Anna Margareth Abdallah (Mb), kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kutoa ushauri, maelekezo na kufuatilia utekelezaji wa shughuli za   Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

4.    Mheshimiwa Spika,kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kuwashukuru wajumbe wa Kamati yako ya Ulinzi na Usalama kwa kutenga muda wao adhimu kwenda kuwatembelea wanajeshi wetu wanaotekeleza jukumu zito la kimataifa la Ulinzi wa Amani huko Darfur nchini Sudan.Naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa ziara yao hiyo ilileta hamasa na kuongeza ari kubwa kwa wapiganaji  wetu katika utendaji wao wa kazi.  Ni matumaini yangu kuwa Kamati itaendelea kufanya ziara kama hiyo katika vikosi vyetu vingine vilivyopo nje ya nchi ikiwemo Force Intervention Brigade (FIB) iliyopo  huko Mashariki mwa Kongo. Aidha, namshukuru mtangulizi wangu, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (Mb), kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi chake cha uongozi wa Wizara.

5.    Mheshimiwa Spika,katika kipindi cha mwaka 2013/14 Wabunge wenzetu waliaga dunia. Wabunge hao ni Mheshimiwa Dkt. William Augustao Mgimwa aliyekuwa Mbunge wa Kalenga na Waziri wa Fedha na Mheshimiwa SaidRamadhanBwanamdogo aliyekuwa Mbunge wa Chalinze.Napenda kuungana na wenzangu walionitangulia kutoa pole za dhati kwako Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, ndugu, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na wapendwa hao. Namuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za Marehemu Peponi. Amina.

DIRA, DHIMA, MALENGO NA MAJUKUMU YA WIZARA YA ULINZI NA JKT

6.    Mheshimiwa Spika,Dira ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inaendelea kuwa ile ile ya kuwa Taasisi iliyotukuka ya kudumisha amani na usalama wa Taifa. Vivyo hivyo, Dhimaya Wizara hii bado ni kulinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya adui wa aina yoyote kutoka ndani au nje ya nchi na kuhakikisha kuwa mamlaka ya nchi (national sovereignty)  na maslahi ya Taifa letu (national interests) yako salama.

7.    Mheshimiwa Spika,ili kufikia Dhima yake, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ina malengo yafuatayo: -

                      i.           Kuwa na Jeshi dogo la Ulinzi wa nchi lenye taaluma, zana na vifaa vya kisasa.  

                    ii.           Kujenga na kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi na makazi.

                   iii.           Kuendeleza utafiti na uhawilishaji wa teknolojia ya kijeshi katika mashirika ya Mzinga na Nyumbu.

                   iv.           Kujenga uzalendo, ukakamavu, maadili mema na utaifa kwa vijana wa kitanzania.

                     v.           Kuimarisha jeshi la akiba.

                   vi.           Kuimarisha mawasiliano salama jeshini.

                  vii.           Kuimarisha umiliki wa ardhi kwa ajili ya matumizi ya jeshi.

                 viii.           Kudumisha amani na usalama kwa kushirikiana na nchi nyingine duniani.

8.    Mheshimiwa Spika, ili kufikiwa kwa malengo yaliyoainishwa, Wizara imekusudia kutekeleza majukumu yafuatayo:-

                      i.        Kuandikisha wanajeshi wa kutosha wenye sifa zinazohitajika kwa ajili ya ulinzi wa Taifa na kuwapatia mafunzo na mazoezi ya kinadharia na kivitendo.
                    ii.        Kuwapatia wanajeshi makazi, zana, vifaa na vitendea kazi bora na vya kisasa.
                   iii.        Kusimamia matunzo na matumizi mazuri ya zana, vifaa na vitendea kazi.
                   iv.        Kuimarisha mafunzo na mazoezi ya kijeshi na kuendesha mafunzo ya ulinzi wa mgambo.
                     v.        Kuendeleza mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria na ya kujitolea ili kuwaandaa kwa ukamilifu vijana wa Kitanzania na kuwajengea moyo wa uzalendo na mshikamano wa kitaifa katika kutekeleza shughuli za kujitegemea.
                   vi.        Kuendeleza utafiti na  uhawilishaji wa teknolojia za kijeshi na kuzalisha mali kupitia mashirika ya Mzinga na Nyumbu.
                  vii.        Kuliwezesha Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) liweze kuzalisha kwa tija na faida itakayochangia katika uendeshaji wa shughuli za Jeshi la Kujenga Taifa.
                 viii.        Kushirikiana na Mamlaka za kiraia katika kukabiliana na majanga ili kuwapatia wahanga misaada ya kibinadamu.
                   ix.        Kuimarisha mazingira bora ya kufanyia kazi na
                     x.        Kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine duniani katika masuala ya kijeshi

UTEKELEZAJI WA MAONI NA USHAURI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA ULINZI NA USALAMA

9.     Mheshimiwa Spika,wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ilipokaa na kujadili Makadirio ya Mapato, Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka 2013/14 ilitoa maoni, ushauri na maelekezo kadhaa kwa Wizara hii yaliyolenga kuboresha utendaji wa majukumu yake. Napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewa yamefanyiwa kazi na majibu yake yameainishwa katika Kiambatanisho Namba 1. Aidha, hoja mbalimbali zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakati wa mjadala huo pia zimezingatiwa katika mpango na bajeti ya mwaka 2014/15 ninayowasilisha leo hapa Bungeni.


HALI YA USALAMA WA MIPAKA MWAKA 2013/14


10.       Mheshimiwa Spika, hali ya usalama wa mipaka ya nchi yetu (nchi kavu, maji na anga) kwa mwaka 2013/14 ilikuwa shwari kwa ujumla. Licha ya kuwepo kwa matishio na mashambulizi ya kigaidi katika eneo la Afrika Mashariki, hakukujitokeza tukio lolote la uharamia kwa upande wa bahari yetu. Hata hivyo, vitendo vya usafirishaji wa madawa ya kulevya na biashara haramu ya usafirishaji binadamu vilijitokeza. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na vyombo vingine vya Usalama  vimeendelea kushirikiana katika kukabiliana na hali hiyo. Kwa upande wa mipaka, matukio ya uharibifu wa alama za mipaka na ujenzi holela unaofanywa na wananchi wanaoishi maeneo ya mipakani hususan maeneo ya Namanga, Jasini, Tunduma na Mtukula yameendelea kujitokeza. Hata hivyo, vikao vya wataalamu kutoka Serikali za Tanzania na nchi jirani za Kenya, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia vyenye lengo la kutatua matatizo hayo vimeanza.  Kufuatia vikao hivyo, alama nane za mpaka (umbali wa km 14.8) zilizokuwa zimeharibiwa katika Wilaya za Tarime (Tanzania) na Kurya (Kenya) zimeimarishwa, ambapo alama saba zimejengwa upya na moja imekarabatiwa. Aidha, alama mpya sabini zimejengwa katikati ya beacons za zamani ili kufanya mpaka huo uonekane kwa urahisi. Mazungumzo kuhusiana na utata wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika  ziwa Nyasa yanaendelea chini ya uratibu wa Wizara ya Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pamoja na hali hiyo, hakuna uhasama wowote wa kijeshi uliojitokeza baina ya nchi zetu.


MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2013/14

11.       Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2013/14 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilikadiria kukusanya mapato ya jumla ya shilingi 68,206,000.00 kutoka katika Mafungu yake matatu ya 38-NGOME, 39-JKT na 57-Wizara. Hadi kufikia mwezi Machi, 2014 Mafungu hayo yalikusanya mapato ya jumla ya shilingi 43,317,624.00 sawa na asilimia 63.5ya makadirio.

12.       Mheshimiwa Spika,katika Mwaka wa Fedha 2013/14, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliidhinishiwa jumla ya shilingi 1,102,999,529,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo katika Mafungu yake matatu. Kati ya fedha hizo, shilingi 857,417,502,000.00 zilitengwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na shilingi 245,582,027,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. Hadi kufikia mwezi Machi 2014, Wizara ilikuwa imepokea jumla ya shilingi 768,496,687,343.00 (sawa na asilimia 69.7) ya bajeti yake. Kati ya fedha hizo shilingi 719,118,556,008.00zilikuwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida (sawa na asilimia 83.8)ya fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya matumizi hayo. Kwa upande wa Matumizi ya Maendeleo, fedha zilizopokelewa ni shilingi 49,378,131,335.00 (sawa na asilimia 20.1) ya fedha zote zilizoidhinishwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Mchanganuo wa Matumizi ya Kawaida na Maendeleo kwa Mafungu yote matatu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa hadi mwezi Machi, 2014 umeonyeshwa katika Kiambatanisho Namba 2.

13.       Mheshimiwa Spika, tathmini ya fedha zilizopokelewa inaonesha kwambamwenendo wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida katika kipindi hicho kiujumla ulikuwa ni wa kuridhisha.  Fedha kwa ajili ya mishahara na marupurupu zilipokelewa kulingana na makisio ya bajeti. Hata hivyo, fedha zilizotolewa kwa ajili ya shughuli  za Maendeleo hadi kufikia mwezi Machi, 2014 zilikuwa kidogo ukilinganisha na mahitaji. Hali hii imeathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Shughuli za Matumizi ya Kawaida

14.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali ili kufikia malengo niliyoyaeleza hapo awali. Shughuli hizo ni pamoja na za:- kulipa stahili mbalimbali za wanajeshi, watumishi wa Umma na vijana walioko katika mafunzo ya JKT; kusafirisha wastaafu; na kutoa huduma muhimu za chakula, tiba na sare. Wizara pia ilipanga kulipia huduma za umeme, maji, simu na mafuta kwa ajili ya uendeshaji wa majukumu ya ulinzi zikiwemo za mafunzo ya kijeshi, mafunzo ya ulinzi wa mgambo na kutengeneza vifaa na zana za kijeshi.



Mafunzo na Mazoezi ya Kijeshi

15.       Mheshimiwa Spika, uimara wa jeshi lolote duniani unategemea mafunzo pamoja na mazoezi ya mara kwa mara. Katika mwaka 2013/14 jeshi letu lilipata fursa ya kushiriki mazoezi mbalimbali ya pamoja na nchi marafiki. Miongoni mwa mazoezi hayo ni zoezi la Kituo cha Uamrishaji (Command Post Exercise - CPX). Zoezi hilo la uamrishaji lilikuwa ni sehemu yamaandalizi ya zoezi la medani  litakalohusisha Majeshi ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zoezi hilo lijulikanalo kwa jina la USHIRIKIANO IMARA 14 (Field Tactical Exercise - FTX),litafanyika katika jimbo la Mwaro nchini Burundi tarehe 13 – 26 Oktoba, 2014.  Aidha, kupitia Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Jeshi letu limeshiriki katika mazoezi ya:- “EX WILWETSCHIA” lililofanyika mwezi Septemba, 2013 nchini Namibia; “EX BLUE ZAMBEZI” lililofanyika nchini Angola mwezi Oktoba, 2013; na “EX CUTLASS EXPRESS” lililofanyika mwezi Novemba, 2013 nchini Seychelles.  Jeshi  linategemea pia kushiriki katika zoezi linaloandaliwa na Umoja wa Afrika (AU). Zoezi hilo lijulikanalo kwa jina la Amani Afrika IIFTX litafanyika nchini Lesotho mwezi Oktoba/Novemba 2014. Mazoezi ya namna hii siyo tu yameimarisha jeshi letu kimedani, bali pia yamekuwa chachu kubwa ya kuboresha mahusiano na majeshi mengine.

(i)            Mafunzo ya Ulinzi wa Mgambo

16.       Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeendelea kuweka umuhimu katika mafunzo ya mgambo. Katika kipindi hiki Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vya Usalama limeendesha mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa wananchi 13,484 (Wanaume 12,337 na wanawake 1,147) ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.8 ikilinganishwa na mwaka 2013. Natoa wito kwa Viongozi wa Wilaya na Mikoa kuongeza kasi ya usimamizi na ushiriki wa mafunzo hayo na kutoa huduma stahiki za usafiri kwa wakufunzi wetu, hifadhi ya silaha na maeneo ya mafunzo. Matarajio ya baadaye ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania ni kuanzisha rasmi Kamandi ya Jeshi la Akiba.

(ii)  Huduma za Afya na Tiba

17.       Mheshimiwa Spika, pamoja na majukumu ya kiulinzi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeendelea kutoa huduma za tiba kwa maafisa, askari, watumishi wa Umma, familia za wanajeshi na wananchi kwa ujumla. Huduma hizo zimezidi kuimarika baada ya kuboresha hospitali za JWTZ zilizoko Mwanza, Mbeya, Bububu (Unguja), Tabora, Nyumbu (Pwani) na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (Arusha).  Lengo letu ni kuboresha huduma hiyo pia katika ngazi ya vituo vya afya vikosini. Ningependa Bunge lako Tukufu litambue kwamba asilimia 80 ya wagonjwa wanaohudumiwa na hospitali na vituo vyetu ni wananchi wanaoishi maeneo jirani.

(iii)         Ushirikiano wa Kiulinzi na Kijeshi na Nchi Nyingine

18.       Mheshimiwa Spika, ushirikiano kati ya nchi yetu na nchi nyingine katika nyanja za kijeshi ni suala muhimu katika mustakabali wa ulinzi na usalama duniani. Hivyo basi, nchi yetu inaendelea kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiulinzi (Bilateral Cooperation) na nchi mbalimbali zikiwemo: - China, Ujerumani, Marekani, Afrika ya Kusini, India, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uingereza, Canada na Urusi. Kupitia ushirikiano huo, Jeshi letu, pamoja na mambo mengine limenufaika katika maeneo yakiwemo ya nyanja za mafunzo ya kijeshi na kitaaluma, zana na vifaa, mazoezi na michezo. Kwa ujumla ushirikiano huu umekuwa ni wa manufaa makubwa.

19.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Serikali imeendelea kudumisha ushirikiano katika Jumuiya za kikanda (Regional Cooperation) hususan za Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Afrika (SADC). Ushirikiano huo ulijikita katika nyanja za mafunzo, mazoezi na michezo baina ya majeshi ya nchi zetu. Na kama nitakavyoeleza hapo baadaye, Tanzania, tukiwa wanachama wa nchi za SADC tumepeleka nchini DRC kikosi cha ulinzi wa amani kuungana na majeshi ya Umoja wa Mataifa. Aidha, kupitia vyuo vyetu, Jeshi letu limeendelea kutoa nafasi za mafunzo ya kijeshi kwa Majeshi ya nchi za Botswana, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Namibia, Seychelles, Swaziland na Zimbabwe kupitia:- Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College- NDC); Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (Command and Staff College-CSC); na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (Tanzania Military Academy-TMA).  Vivyo hivyo, Maafisa wetu nao walipata mafunzo katika baadhi ya nchi hizo.

20.       Mheshimiwa Spika, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendeleakushiriki katikaOperesheni za Ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali. Hadi sasa, ushiriki wa wanajeshi wetu katika Operesheni hizo ni kama ifuatavyo;

                      i.        Kikosi kimoja (TANZBATT – 8) kipo Darfur nchini Sudan.
                    ii.        Kikosi kimoja (TANZBATT – 1) kipo Mashariki mwa DRC ikiwa ni sehemu ya MONUSCO Force Intervention Brigade.
                   iii.        Kombania mbili za Polisi Jeshi zipo nchini Lebanon.
                   iv.        Waangalizi wa amani (military observers)  na maafisa wanadhimu (staff officers) wapo katika baadhi ya nchi ikiwemo Sudani Kusini. 

(iv)         Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Vijana


21.       Mheshimiwa Spika, Jeshi la Kujenga Taifa limeendelea kutoa mafunzo kwa vijana wa kujitolea na wa Mujibu wa Sheria. Malengo ya mafunzo hayo ni pamoja na kujenga uzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa na kuwapa stadi za maisha vijana wa kitanzania. Katika mwaka 2013/14 JKT linaendesha operesheni moja ya mafunzo ya vijana wa kujitolea ijulikanayo kama Operesheni Miaka Hamsini ya Muungano. Katika operesheni hii idadi ya vijana 8,439 (wavulana 6,610 na wasichana 1,829) wanaendelea na mafunzo yaliyoanza mwezi Machi 2014. Nafurahi kulieleza Bunge lako Tukufu kwamba hivi sasa vyombo vya Ulinzi na Usalama vimeanza kutekeleza utaratibu wa kuajiri vijana waliopitia mafunzo ya JKT. Idadi ya vijana  7,062 walichukuliwa  na vyombo hivyo kwa mwaka huu. Aidha, vijana 155 walichukuliwa na taasisi na makampuni binafsi (Benki Kuu ya Tanzania-BOT, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania-TAA, Barrick  Gold Mine na Geita Gold Mines).

22.       Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mafunzo ya Mujibu wa Sheria,  na kama ilivyoelezwa mwaka jana, mafunzo hayo yalirejeshwa kwa wahitimu wa kidato cha sita kuanzia mwezi Machi 2013. Mafunzo haya yaliendelea kutolewa ambapo jumla ya vijana 10,505 wameweza kuhitimu mafunzo hayo kipindi hiki. Kati yao, vijana 9,510 walihitimu mafunzo awamu ya pili iliyomalizika mwezi Oktoba, 2013. Ingawa mategemeo yalikuwa kuchukua idadi ya vijana 15,000 wajiunge na mafunzo awamu ya tatu, ni vijana 1,002 waliweza kujiunga na mafunzo hayo yaliyoanza mwezi Oktoba, 2013 hadi Januari 2014, ambapo vijana 995 ndio waliohitimu. Kupatikana kwa idadi ndogo ya vijana wa awamu ya tatu na kutopatikana kabisa kwa vijana awamu ya nne kulitokana na vijana wengi kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ambapo muhula wa masomo huanza mwezi Oktoba.

23.       Mheshimiwa Spika, utaratibu wa vijana waliomaliza kidato cha sita kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria si wa hiari. Hivyo kwa mwaka huu Jeshi la Kujenga Taifa litachukua vijana wasiopungua 45,000 watakaomaliza kidato cha sita hivi karibuni.  Awamu ya kwanza kwa mwaka 2014/15 itaanza mwezi Juni hadi Septemba, 2014 na itahusisha vijana 20,000.  Awamu ya pili itakayochukua vijana 14,450  itaanza mwezi Oktoba 2014 hadi Januari 2015.  Na awamu ya tatu itakayochukua vijana 10,550 itaanza mwezi Januari hadi Aprili 2015. Naomba vijana wote wanaotakiwa kujiunga na mafunzo ya JKT watambue kuwa ni kosa kisheria kukaidi wito wa kujiunga na mafunzo hayo.

(v)           Mapambano dhidi ya UKIMWI

24.       Mheshimiwa Spika, UKIMWI umeendelea kuwa janga la kitaifa na kuleta athari kubwa kijamii, kiuchumi na kuathiri nguvu kazi inayotegemewa. Hivyo, jitihada za kupambana na maambukizi ya UKIMWI ni suala endelevu. Kwa msingi huo Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeendelea kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga ili kuzuia maambukizi mapya. Aidha, wizara imekuwa ikihimiza upimaji wa hiari kwa maafisa, askari na watumishi wa umma na vijana wa JKT kwa kutumia waelimishaji rika. Kwa wale ambao tayari wameshaambukizwa virusi vya UKIMWI, Wizara imeendelea kutoa huduma ya  lishe na dawa za kupunguza makali ya virusi (ARVs).

Shughuli za Matumizi ya Maendeleo

25.       Mheshimiwa Spika,utekelezaji wa shughuli za maendeleo hadi kufikia robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2013/14 kwa ujumla haukuwa mzuri. Mafungu yote matatu yalipokea wastani wa asilimia 20.1 ya bajeti iliyoidhinishwa.Kwa mapokezi hayo, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeweza kutekeleza miradi ifuatayo; mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 za makazi ya wanajeshi, kulipia madeni ya kimikataba, kukarabati majengo pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na makazi katika makambi na viteule vya JKT, ulipiaji fidia kwa maeneo yaliyotwaliwa na Jeshi, kuboresha mawasiliano jeshini, ujenzi wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi Kihangaiko, kulipia ujenzi wa viporo vya miradi ya maji Msangani na Ngerengere na ukarabati wa viteule vya Kasanga, Kalando na Hospitali ya Jeshi Lugalo, kuboresha miundombinu ya Shirika la Nyumbu na ununuzi wa malighafi kwa Shirika la Mzinga.
(i)            Ujenzi wa Nyumba na Makazi ya Wanajeshi

26.       Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2013/14, Wizara yangu ililiarifu Bunge lako Tukufu kwamba, maandalizi ya ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania yamekamilika ambapo ujenzi wa nyumba 6,064za awamu ya kwanza ungeanza. Nafurahi kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa ujenzi wa nyumba hizo unaotekelezwa na Kampuni ya Shanghai Construction (Group) General Company ulianza rasmi tarehe 17 Julai, 2013. Ujenzi huo utakaofanyika katika vikosi 37 vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Kujenga Taifa utakuwa katika mikoa tisa kwa mgawanyo ufuatao; Arusha (792), Dar es Salaam (2,288), Dodoma (592), Kagera (144), Morogoro (616), Pemba (320), Pwani (840),Kigoma (160) na Tanga (312). Ujenzi huu utachukua muda wa miezihamsini (50). Hadi sasa, ujenzi tayari umeanza kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambapo hatua ya ujenzi huo imefikia asilimia 80. Maandalizi ya ujenzi katika mikoa ya Arusha, Morogoro, Pemba na Tanga unaotarajiwa kuanza mwezi Juni 2014yamekamilika.

(ii)          Ununuzi wa Zana na Vifaa vya Kijeshi

27.       Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na azma yake ya kuimarisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kulipatia zana na vifaa vya kisasa. Katika mwaka 2013/14 Jeshi lilipokea zana na vifaa vya kisasa ambavyo vimeendelea kutumika katika shughuli za ulinzi na mafunzo. Nisingependa kuwachosha Waheshimiwa Wabunge katika eneo hili kwani mwenye macho alijionea mwenyewe yaliyojiri siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano tarehe 26 Aprili, 2014.  Kwa yule ambaye hakubahatika kuyaona, ni imani yangu kuwa alisimuliwa.  Mpango wa ununuzi wa zana za kisasa na bora ni endelevu, hivyo natarajia Bunge lako Tukufu litaendelea kuidhinisha fedha za kutekeleza mpango huu.

 (iii)     Shirika la Uzalishaji Mali la SUMAJKT


28.       Mheshimiwa Spika, Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT) linaendelea kutekeleza majukumu yake kupitia idara zake za uhandisi na ujenzi, viwanda na kilimo, biashara na utalii.  Utekelezaji wa shughuli hizi unalenga katika kuhakikisha kuwa SUMAJKT inafanikisha malengo iliyojiwekea kwa tija na ufanisi mkubwa. Katika kutekeleza azma  ya kujitosheleza kwa chakula, mwaka 2013/14 SUMAJKT lilifanikiwa kulima ekari 4,390 za mazao mbalimbali ya chakula na ekari 1,913 za mbegu bora.  Tatizo linaloendelea kulikabili SUMAJKT katika eneo hili ni kutokulipwa madeni. Hadi sasa jumla ya shilingi 495,792,000.00 hazijalipwa na makampuni yaliyouziwa mbegu hizo. Makampuni hayo ni Agricultural Seed Agency (ASA), Tropical Seed Co. Ltd na Southern Highland Seed Growers Ltd.

29.       Mheshimiwa Spika, SUMAJKT kupitia “National Service Construction Department” inatekeleza miradi  ya ujenzi wa majengo na barabara. Katika kipindi cha mwaka 2013/14 Jeshi la Kujenga Taifa limefanya mageuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha ujuzi wa wataalam, kuongeza matumizi ya zana na mitambo pamoja na kuimarisha uwezo wa Idara zake ili kujikita kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa majengo na barabara. Miongoni  mwa miradi inayotekelezwa ni ya ujenzi wa Shule ya  Mafunzo ya Awali  (Recruits Training School - RTS) Kihangaiko, ujenzi wa barabara kiwango cha lami wilayani Chato, ujenzi wa barabara za ndani katika mgodi wa Tulawaka na ukarabati wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

30.       Mheshimiwa Spika, katika eneo la ulinzi wa mali za wananchi, SUMAJKT limejizatiti katika shughuli za ulinzi kupitia kampuni tanzu ya SUMAJKT Guard Ltd. Vijana wanaotoa huduma hii ni wale waliohitimu mafunzo ya JKT ambao sasa wanafikia idadi ya 1,668. Hadi sasa SUMAJKT Guard Ltd wameweza kupata zabuni ya kutoa huduma hiyo ya ulinzi kwa taasisi za Serikali, mashirika ya Umma na binafsi, viwanda na migodi. Katika  mwaka 2014/15 Kampuni hii inatarajia kuajiri vijana 2,000 kuongeza idadi ya nguvu kazi iliyopo na hivyo kupanua utoaji huduma hiyo katika taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

31.       Mheshimiwa Spika, kama ilivyoelezwa katika hotuba ya mwaka 2013/14 kuhusiana na mradi wa matrekta, matrekta 1,558 na zana za kilimo zenye thamani ya shilingi 53,675,837,001.00 ziliuzwa kwa mkopo kwa wadau mbalimbali zikiwemo Halmashauri za Wilaya, vikundi vya uzalishaji mali, SACCOS na watu binafsi wakiwemo baadhi ya Waheshimiwa Wabunge.  Marejesho ya mikopo hii  hadi kufikia Machi, 2014 ni kiasi cha Shilingi 26,162,374,328.96. Baada ya mauzo ya awamu ya kwanza kukamilika, SUMAJKT bado limeendelea kutekeleza mradi wa uagizaji wa matrekta mengine pamoja na zana za kilimo. Hivi sasa yapo matrekta 197 aina ya New Holland na Farmtrac kwenye kituo cha Mwenge. Waheshimiwa Wabunge, Halmashauri za Wilaya, vikundi vya uzalishaji mali, SACCOS na watu binafsi  wenye mkopo mnakumbushwa kurejesha mikopo yenu na mnahamasishwa kuja  kununua matrekta mapya.

(i)            Shughuli za Shirika la Mzinga


32.       Mheshimiwa Spika, shughuli za msingi za Shirika la Mzinga na kampuni yake tanzu ya Mzinga Holdings zimeendelea kwa mafanikio. Uzalishaji wa mazao ya risasi na milipuko umeongezeka ikiwa ni pamoja na kupata masoko mapya ya mazao hayo nje ya nchi. Aidha, katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki, Shirika la Mzinga limeteuliwa kuwa Centre of Excellence. Kwa upande wa Mzinga Holdings shughuli zake zimejikita katika ujenzi na ukarabati wa majengo na uendeshaji wa maduka ya kuuza bidhaa zisizolipiwa kodi (Duty Free Shops) kwenye vikosi na makambi ya Jeshi.

(ii)           Shughuli za Shirika la Nyumbu

33.       Mheshimiwa Spika,shughuli za utafiti katika Shirika la Nyumbu hazikuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutopatikana kwa fedha za maendeleo. Hivyo tafiti zinazohusiana na mitambo ya kuchuna mkonge, “engine” na “gear box” za matrekta madogo na uzalishaji wa vipuri vya mashine (prototype) na pampu ya umwagiliaji hazikukamilika. Hata hivyo, shughuli za uzalishaji vipuri mbalimbali ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa vipuri vya Shirika la Reli (TRL) hususan “brake blocks” zimeendelea. Aidha, Shirika limeendelea kutoa huduma ya kutengeneza pampu za maji za DAWASCO na pia kuhusika katika ufungaji na ukarabati wa vifaa vinavyotumiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya Ulinzi wa Amani huko Darfur - Sudan, Lebanon na Mashariki mwa DRC. Miongoni mwa vifaa vilivyofanyiwa ukarabati na Nyumbu ni magari ya kubebea mizigo, maji, mafuta na askari. Aidha, uzalishaji na upatikanaji wa “Powered Brick making machine”, mashine za kusaga na kukoboa nafaka unaendelea.

(iii)          Mtandao wa Mawasiliano Jeshini

34.       Mheshimiwa Spika, kazi ya ukarabati na uboreshaji wa mawasiliano jeshini imeendelea kutekelezwa. Awamu ya kwanza ya mradi wa uboreshaji wa mawasiliano ndani ya vikosi imekamilika katika mkoa wa Dar es Salaam. Kazi ya uboreshaji wa mawasilianao ndani ya vikosi vilivyo nje ya Mkoa wa Dar es Salaam haijafanyika kutokana na kutokupatikana kwa fedha za maendeleo. Hivyo utekelezaji wa kazi hiyo pamoja na awamu ya pili ya kuunganisha mfumo wa Satellite utategemeana na upatikanaji wa fedha. Zoezi la kusimika minara ya mawasiliano huru na salama nchi nzima linaendelea.

(iv)          Uvamizi wa Maeneo ya Jeshi, Upimaji na Ulipaji Fidia


35.          Mheshimiwa Spika, tatizo la uvamizi wa maeneo ya Jeshi bado linaendelea kujitokeza. Katika kipindi hiki maeneo yaliyoathirika na tatizo hilo ni pamoja na Tondoroni – Pwani, Tanganyika Packers na Monduli –Arusha, Kimbiji – Dar es Salaam, Chita – Morogoro, Itaka na Uyole – Mbeya, Uwanja wa Ndege na Ilemela – Mwanza na Kisakasaka - Unguja.  Pamoja na hatua zinazochukuliwa zikiwemo za kisheria, nawasihi wananchi wasivamie maeneo ya Jeshi wala kuendesha shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo.

36.       Mheshimiwa Spika, kuhusu fidia, katika mwaka 2013/14 Wizara imekamilisha kulipa fidia katika maeneo yafuatayo; Mwakidila (Tanga), Cheyo (Tabora), Mwantini (Shinyanga) na Mataya Kiromo (Pwani).  Mipango yetu ya kulipa fidia katika maeneo mengine yaliyochukuliwa kwa matumizi ya Jeshi inaendelea. Aidha, maeneo tunayoyalenga kulipa fidia katika mwaka 2014/15 ni ya Makambako (Njombe), Ilemela na Kigongo Ferry (Mwanza). Zoezi la kupima na kuweka alama za mipaka, mabango na “buffer zones” linaendelea.

CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2013/14

37.       Mheshimiwa Spika,changamoto kubwa katika utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2013/14 ni ya Wizara kuidhinishiwa kiwango kidogo cha bajeti ikilinganishwa na mahitaji halisi. Kwa mfano katika mwaka wa fedha 2013/14 wakati mahitaji halisi kwa kuzingatia vipaumbele vya Wizara yalikuwa ni shilingi 1,741,888,249,500.00, bajeti iliyoidhinishwa ilikuwa shilingi 1,102,999,529,000.00 sawa na asilimia 63.3 ya mahitaji. Hali hiyo imepelekea utekelezaji wa shughuli za Wizara hususan shughuli za maendeleo kutofikia malengo yaliyokusudiwa. Baadhi ya shughuli zilizoathirika ni za uboreshaji wa viwanda, utafiti na uzalishaji wa bidhaa za kijeshi, kulipia huduma na mahitaji muhimu kama vile mafuta, maji na umeme. Hali hiyo imesababisha Wizara kulimbikiza madeni makubwa ya kimkataba.Kwa upande wa matumizi ya kawaida, changamoto hii imesababisha ongezeko kubwa la madeni yakiwemo ya wazabuni na ya taasisi zinazotoa huduma muhimu za maji, umeme na simu.

38.       Mheshimiwa Spika, changamoto nyingine inayoikabili Wizara ni mtiririko wa fedha kutoka Hazina kutozingatia mpango kazi wa Wizara, ambapo fedha zinapoidhinishwa, hutolewa zikiwa pungufu na bila kuzingatia ratiba ya mikataba.  Hali hii imesababisha shughuli za Wizara hususan za maendeleo kutotekelezwa kama ilivyopangwa. Matokeo yake ni kuwa  Wizara imeshindwa kukamilisha ujenzi wa majengo na miundombinu katika makambi, kushindwa kulipa mikopo mbalimbali ukiwemo wa NSSF na kushindwa kulipa malipo ya kimikataba.

MPANGO WA MWAKA 2014/2015
 
39.       Mheshimiwa Spika, mpango wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka 2014/15 umekusudia kuimarisha utendaji kazi na ufanisi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika kutekeleza majukumu ya Ulinzi wa Taifa kulingana na Dira, Dhima na Malengo ya Wizara. Vilevile, mpango umelenga kuimarisha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa vijana wa Mujibu wa Sheria na wale wa kujitolea. Aidha, Wizara inakusudia kukamilisha miradi inayoendelea na kulipa madeni ya kimikataba. Hivyo, Wizara  imepanga kutekeleza shughuli zifuatazo:-

i.        Kununua vifaa na zana za kijeshi ikiwemo vifaa vya uhandisi wa medani na ndege vita.
ii.            Kuanza ujenzi wa gati katika Kamandi ya Jeshi la Wanamaji.
iii.           Kuboresha mifumo ya mawasiliano ya ndani na nje ya vikosi na makambi ya Jeshi.
iv.           Kuendelea na ujenzi wa nyumba 6,064 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi.
v.             Kukamilisha ujenzi wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS) – Kihangaiko Pwani na Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) – Tengeru Arusha.
vi.           Kuboresha viwanda vya  Mashirika ya Mzinga na Nyumbu.
vii.          Kulipa mkopo wa NSSF wa ujenzi wa nyumba za makazi ya wanajeshi.
viii.         Upimaji na ulipaji wa fidia ya ardhi katika maeneo ya wananchi yaliyochukuliwa kwa ajili ya matumizi ya Jeshi.
ix.           Kuanza ujenzi wa Hospitali Kuu ya Jeshi huko Mataya - Kiromo Pwani.
x.             Ujenzi na umaliziaji wa viporo vya nyumba, bwalo na bweni huko Pemba.
xi.           Ujenzi wa maghala ya kuhifadhia silaha na zana pamoja na kuboresha mawasiliano.
xii.          Kulipia gharama za matumizi ya mahitaji muhimu ya umeme, maji, simu na huduma za uendeshaji wa majukumu ya kimsingi.
xiii.         Kulipia stahili mbalimbali za wanajeshi, vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa na Watumishi wa Umma.
xiv.         Kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine duniani katika nyanja za kijeshi na ulinzi.
xv.          Kulipa madeni ya  kimkataba.
xvi.         Kuongeza uwezo wa makambi ya JKT kuweza kuchukua idadi kubwa ya vijana kwa wakati mmoja.
xvii.        Kupanua wigo wa makundi ya vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.

SHUKRANI

40.       Mheshimiwa Spika, kabla sijahitimisha hotuba yangu napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru  wafuatao kwa michango yao katika maandalizi ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu:- Katibu Mkuu Bw. Job D. Masima; Naibu Katibu Mkuu Bi. Mwintango Rose Shelukindo; Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis A Mwamunyange; Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Samuel A Ndomba; Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M Muhuga; Wakuu wa Kamandi za Jeshi la Nchi Kavu Meja Jenerali Salum M Kijuu; Jeshi la Anga Meja Jenerali Joseph F Kapwani na Jeshi la Wanamaji Brigedia Jenerali Rogastian S Laswai; Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga Meja Jenerali Dkt Charles N Muzanila na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumbu Kanali John K Nchimbi.

41.       Mheshimiwa Spika, pia napenda kuwashukuru Wakuu wa Idara na Vitengo (Makao Makuu ya Wizara), Wakuu wa Matawi (NGOME), Wakuu wa Idara (Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa), Maafisa na Askari na Watumishi wa Umma wa Wizara kwa kunipokea na kunipa ushirikiano katika kufanikisha majukumu ya Wizara.  Vile vile, naomba kuwashukuru wapiga kura wangu wa jimbo la Kwahani kwa ushirikiano wao walionipa katika mwaka 2013/14. Ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana zaidi kwa manufaa ya jimbo letu na Taifa kwa ujumla. Aidha, namshukuru Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali na watumishi walio chini yake kwa kuchapisha Hotuba hii kwa wakati.

42.          Mheshimiwa Spika,kwa umuhimu wa pekee na kwa kupitia Bunge lako Tukufu naomba kuwasilisha salamu za pongezi maalum za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa wanajeshi wote kwa kufanikisha maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. Kazi waliyoifanya ni kubwa na waliifanikisha kwa weledi, utii, uhodari, ujasiri na kwa kishindo cha hali ya juu. Ushiriki wao huo umeudhihirishia umma wa Watanzania na ulimwengu kwa ujumla kuwa jeshi letu ni imara, shupavu na lipo tayari kulinda, kutetea na kudumisha Muungano wetu. Nami nikiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa natamka kuwa ‘I am proud of our gallant men and women in uniform’.

43.       Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia na kwa niaba ya wanajeshi wote namshukuru sana Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Hiba (legacy) yake ya  uongozi, ushupavu, uvumilivu na maridhiano itakumbukwa na kuenziwa vizazi na vizazi hususan kwetu sisi wanajeshi.   Ahadi yetu kwake ni kuwa tutaendelea kusimama imara, kupokea na kutii amri na maelekezo yake bila hila yoyote na kutoyumbishwa na kauli potovu za kisiasa.

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI YA MWAKA 2014/15

i.              Makadirio ya Mapato

44.          Mheshimiwa Spika,vyanzo vya mapato ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Taasisi zake bado ni vidogo.  Chanzo kikuu  cha mapato kwa Wizara ya Ulinzi na JKT na taasisi zake kimeendelea  kutegemea uuzaji wa nyaraka za zabuni. Hivyo, makadirio ya  Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2014/15 ni kukusanya mapato yenye jumla ya shilingi 60,506,000.00 kwa mchanganuo ufuatao:

Fungu38 – NGOME                     =            2,001,000.00
Fungu 39 – JKT              =          48,503,000.00
Fungu 57 – Wizara                     =          10,002,000.00
Jumla  shilingi           =          60,506,000.00

ii.            Bajeti ya Matumizi ya Kawaida na Maendeleo

45.       Mheshimiwa Spika, ili Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iweze kutekeleza majukumu yake katika mwaka 2014/15 inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi 1,269,076,056,000.00 ambazo kati yake shilingi 1,020,076,056,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na shilingi 249,000,000,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. Mchanganuo wa bajeti hiyo kwa kuzingatia mafungu ya Wizara ni ufuatao:-





FUNGU 38 NGOME




Matumizi ya Kawaida shilingi
803,542,549,000.00
Matumizi ya Maendeleo shilingi
  12,000,000,000.00
Jumla ya Makadirio kwa Fungu 38 shilingi

815,542,549,000.00


FUNGU 39 JKT

Matumizi ya Kawaida shilingi
196,822,661,000.00
Matumizi ya Maendeleo shilingi    
7,000,000,000.00
Jumla ya Makadirio kwa Fungu 39 shilingi

203,822,661,000.00


FUNGU 57 WIZARA YA ULINZI

Matumizi ya Kawaida  shilingi
19,710,846,000.00
Matumizi ya Maendeleo shilingi
230,000,000,000.00
Jumla ya Makadirio kwa Fungu 57 shilingi

249,710,846,000.00




MWISHO


46.          Mheshimiwa Spika, hotuba hii inapatikana pia katika tovuti ya Wizara (www.modans.go.tz).  Naomba kutoa Hoja.



Viewing all 4100 articles
Browse latest View live




Latest Images