Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

RAIS MUGABE ASAINI MKATABA WA SIRI NA IRAN KUSAFIRISHA URANI...

$
0
0
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, anaonekana hapa akipeana mikono na Rais wa zamani wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad mwaka 2006.
Zimbabwe imesaini mkataba wa siri kusafirisha urani kwenda Iran kwa ajili ya mpango wake wenye utata wa nyuklia, kwa mujibu wa ofisa mmoja wa juu wa Serikali mjini Harare.

Makubaliano kati ya nchi hizo mbili, ambayo yatashuhudia maelfu ya tani za urani ghafi yakisafirishwa kwenda Tehran kwa ajili ya kuboreshwa, yamedaiwa kuendelea kwa miaka miwili, limeripoti gazeti la Times.
Naibu Waziri wa Madini wa Zimbabwe, Gift Chimanikire, alisema 'mkataba wa maridhiano' umesainiwa kati ya nchi hizo mbili ambazo zote zinakabiliwa na vikwazo kimataifa vya kiuchumi.
Iran inasisitiza kwamba mpango wake wa nyuklia unalenga kukidhi mahitaji yake binafsi ya nishati, hatahivyo inaaminika kwa mapana wanatarajia kuunda silaha za nyuklia.
Chimanikire  aliyaelezea madini kama 'tiketi ya Zimbabwe' na kusema idadi ndogo pekee ya maofisa wa serikali walikuwa wakifahamu mkataba huo ambao utaihakikishia nchi hiyo ya Afrika kupokea mabilioni wakati huu ambao inahitaji fedha kwa udi na uvumba.
Alisema kampuni moja ya China imekuwa ikifanya utafiti kwenye eneo lililoko mbali kaskazini mwa Zimbabwe. Alilieleza The Times: "Nimeuona [mkataba wa maridhiano] kwa ajili ya kusafirisha urani kwa Wairani."
Zimbabwe inaaminika kuwa na urani iliyohifadhiwa takribani tani 45,000. Hatahivyo nyingi kati ya hizo zimechangika na madini mengine ikimaanisha itachukua miaka kadhaa kutenganisha na kwa gharama kubwa.
Wachina hao wanaaminika pia kuifuata Zimbabwe na kuipatia msaada wa kifedha na miradi ya ujenzi kwa malipo ya haki za uchimbaji madini nchini humo.
Japo Iran inayo akiba yake yenyewe ya urani si halisi kama zile zinazopatikana katika sehemu nyingine duniani.
Wataalamu wanaamini taifa hilo la Kiislamu tayari limeshatenga kilo 182 za urani safi, lakini litahitaji takribani kilo 250 kuweza kutengeneza bomu la nyuklia.
Rais aliyemtangulia Rouhani, Mahmoud Ahmadinejad, alikutana na Rais Mugabe mwaka 2010, pale kiongozi huyo wa Afrika alipoelezea tamaa ya Iran ya nyuklia kama 'sababu pekee'.
Kabla ya kuachia madaraka mnamo Juni, Ahmedinejad, alifanya safari kwenda Niger, nchi ya nne kubwa duniani kwa uzalishaji wa urani.
Maofisa usalama wa Uingereza walisema walikuwa wakifahamu kwamba Iran inajadiliana na Zimbabwe. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alisema: "Taarifa zozote za urani inayosafirishwa kwenda Iran inashughulikiwa."

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles