Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

ALIYEIBA MTOTO KUOKOA NDOA AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA

$
0
0
Mkazi wa kijiji cha Kisumba, Manispaa  ya Sumbawanga, Halima Nambeya (18)  ametupwa jela mwaka mmoja na Mahakama ya wilaya ya Sumbawanga baada ya kukiri kosa la kuiba mtoto mchanga  wa kiume  kwa lengo la  kulinda ndoa yake  ili  asiachike  kwa kukosa mtoto.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Frednand Rwegasira  alisema mtuhumiwa huyo alimuiba mtoto  huyo  katika eneo la Jangwani mjini hapa  na kumsafirisha  hadi kijijini Kisumba nyumbani kwa babu yake.
“Halima  alifikishwa mahakamani  na kusomewa  mashitaka ya wizi  wa mtoto  na alikiri  kosa lake hilo  na amehukumiwa kutumikia kifungo  cha  mwaka mmoja  jela," alisema.
 “Uchunguzi  wa awali  ulibainisha kuwa Halima awali  alimdanganya mumewe alikuwa mjamzito  hivyo  anadaiwa kumuiba mtoto huyo  mchanga ili  amdanganye mumewe  kuwa amejifungua  kwa lengo la  kulinda ndoa yake  ili  asiachike," alibainisha Kaimu Kamanda huyo.
Kwa mujibu wa Rwegarisa, Halima anadaiwa kutenda kosa hilo  Juni 29 mwaka huu  ambapo  alikamatwa na Polisi  siku nne  baadaye  akiwa nyumbani  kwa babu yake kijijini Kisumba, Manispaa ya Sumbawanga.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

Latest Images

Trending Articles