Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

MFUKO WA AFYA KUCHANGIWA SHILINGI BILIONI 108.5

$
0
0
Wadau wa Maendeleo watachangia Sh bilioni 108.5 kwa ajili ya Mfuko wa Afya kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014/15.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam baada ya kusaini makubaliano, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk Servacius  Likwelile alisema fedha hizo zitatumika katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.
“Fedha hizi zitawezesha utekelezaji wa vipaumbele katika maeneo afya ya uzazi na mtoto, kuimarisha na kudhibiti magonjwa ya kawaida na yale ya milipuko.
“ Pia zitatumika kwa ajili ya kuboresha usimamizi wa huduma za afya katika ngazi zote.”
Aidha, Likwalile aliomba wadau wa maendeleo kutoa fedha hizo mapema ili kuruhusu utekelezaji wa shughuli zilizokubaliwa.
Akizungumzia mgawanyo wa fedha hizo, Likwalile alisema Sh bilioni 80.4 zitatumika na halmashauri katika kutekeleza mipango ya afya ya mwaka wakati Sh bilioni 3.8 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mipango ya afya ya mwaka katika ngazi ya mikoa.
Likwelile alisema Sh bilioni 15.3 zitatumika kwa ajili ya kununua na kusambaza dawa na vifaa tiba kupitia Bohari ya Kuu ya Dawa (MSD) wakati Sh bilioni 8.5 zitatumiwa na Wizara ya Fedha na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Donan Mmbando alisema serikali na wadau wa afya wameandaa mikakati ya kupambana na kuzuia magonjwa ya milipuko ukiwamo ugonjwa wa Ebola.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

Latest Images

Trending Articles