Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal, Kamanda wa Kanda Maalumu Suleiman Kova, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik na maofisa kadhaa wa serikali wakiwamo waandishi wa habari wamenusurika kifo baada ya helikopta ya polisi kuanguka Uwanja wa Ndege wa Julius K. Nyerere, Dar es Salaam muda mfupi uliopita.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Mkuu huyo wa mkoa na msafara wake walikuwa waanze safari ya kukagua athari za mafuriko zilizotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, helikopta hiyo iliruka juu umbali wa futi 15 na kisha kuanguka chini ubavu.
Haikuweza kufahamika mara moja chanzo cha ajali hiyo.
aarifa zaidi endelea kuperuzi ziro99blog.