Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4515

MWENYEKITI, MADIWANI WANUSURIKA SHAMBULIO LA UJAMBAZI KATIKA BAA...

$
0
0
Makamu Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilayani Simanjiro, Jackos Sipitek pamoja na madiwani wawili wa viti maalumu wamenusurika  katika shambulio la majambazi kutaka kuwadhuru polisi kwenye baa ya Pama iliyopo makao mapya jijini Arusha.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika baa hiyo mmoja kati ya madiwani hao, Bahati Patson alisema walifika jijini Arusha juzi kwenye biashara zao na kufikia katika baa hiyo ambayo ndani yake kuna vyumba vya kulala wageni.
Alisema wakiwa katika eneo la baa wakinywa na kula karibu na majambazi hao pasipo kujua, ghafla waliingia polisi wawili waliokuwa wamevaa kiraia wakiwaambia watu hao waliokuwa wanne  mezani wakila nyama kuwa wapo chini ya ulinzi.
Walipoambiwa kuwa wapo chini ya ulinzi ghafla jambazi mmoja alichomoa bastola na kutaka kumrushia risasi na hapo ndipo polisi mwingine aliyekuwa na silaha akaanza kuwarushia risasi huku wateja wa baa hiyo kila mmoja akikimbia na wengine kukimbilia chooni zaidi ya saa mbili.
Naye mmoja kati ya wahudumu hao, Maria Bonde alisema alishukuru polisi walivyofanya kazi yao bila kuleta maafa kwa wateja wao.
"Siwezi kusema ni hasara kiasi gani tumepata lakini ukweli polisi waliweza kuwadhibiti majambazi hao kwa ufundi zaidi kwani kulikuwa na wateja wengi kwenye baa lakini hakuna aliyepata majeraha zaidi ya hao majambazi wenyewe," alisema Bonde.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas  akizungumza na waandishi wa habari jana, alithibitisha  kutokea kwa  tukio hilo juzi saa 1:00  usiku maeneo ya makao mapya  katika baa ya Pama ambapo watu wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wanaokadiriwa kuwa na miaka 25 hadi 35 na majina yao hayajafahamika waliuawa katika majibizano ya risasi na polisi.
Alisema katika tukio hilo askari hao walikamata bastola aina ya Star yenye namba 42640 FNH  model KAL 7.65 ikiwa na risasi tatu katika magazini, maganda matatu ya risasi pamoja na begi moja dogo la mgongoni lenye rangi nyekundu likiwa na risasi na kufanya risasi jumla yake kuwa saba pamoja na dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi(ARVs) zilizokuwa kwenye pakiti.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4515

Trending Articles