![]() |
Wapiganaji wa Intarahamwe. |
Uzinduzi huo ulifanywa Dar es Salaam jana na Balozi wa Rwanda nchini, Ben Rugangazi aliyeeleza kuwa uzinduzi huo ni sehemu ya maandalizi ya kumbukumbu rasmi ya mauaji hayo, itakayofanyika Aprili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Balozi Rugangazi alisema kuwa wana Rwanda wamekuwa na umoja unaowafanya wawe kitu kimoja, hivyo kutofikiria kutengana tena kwa kuendeleza visasi.
Alisema, umoja huo umekuwa ukiendelea kuimarika kila siku, hivyo kuwafanya waliokuwa wakichochea mauaji na hata kuyawezesha kushindwa kupata nafasi ya kuurudia uchochezi wao.
Katika mauaji hayo ya mwaka 1994, kwa mujibu wa taarifa ya Balozi Rugangazi aliyoitoa juzi, watu 10,000 walikuwa wakiuawa kila siku katika kipindi chote cha machafuko.